Msururu wa wapiga kura katika kitongoji cha
Kanyama nje ya jiji la Lusaka leo asubuhi
Leo
wananchi wa Zambia wanafanya Uchaguzi mdogo kumchagua Rais wa sita tangu wa nchi
hiyo tangu ipate uhuru mwaka 1964. Uchaguzi huu unafanyika kufuatia
kifo cha Rais Michael Chilufya Sata, kilichotokea tarehe 28 Oktoba 2014, mjini London
Uingereza alikokwenda kwenye matibabu. Rais Sata aliingia madarakani Septemba
2011.
Mshindi
katika uchaguzi huu atatawala hadi 2016 ambapo utafanyika Uchaguzi Mkuu. Katika
uchaguzi huu wagombea kutoka vyama vya siasa vipatavyo kumi na moja (11) wamejitokeza
kushiriki kama ifuatavyo:
·
Mhe.
Edgar C. Lungu – Chama cha Patriotic Front (PF) –mpaka anapoingia kwenye
kinyangányiro hiki ni Waziri wa Sheria na Waziri wa Ulinzi. Yeye anajaribu
kutetea chama hiki tawala ili kimalizie kipindi kilichobaki.
·
Bw.
Hakainde Hichilema - Chama cha United Party for National Development (UPND) - ambaye anajaribu tena kwa mara
ya nne, anachuana vikali na mgombea wa chama cha PF.
·
Dkt.
Nevers S. Mumba - Chama cha Movement for Multi Party Democracy (MMD)- mgombea wa chama hiki ni ana changamoto kubwa hasa
baada ya wengi wa Wabunge wa chama chake kuamua kumuunga mkono mgombea wa chama
cha UPND.
·
Bw.
Elias Chipimo (jnr) - National Restoration Party (NAREP) - ambaye anashiriki kwenye uchaguzi kwa mara ya pili sasa.
·
Dkt. Ludwig S. Sondashi - Forum for Democratic
Alternatives (FDA) - anashiriki kwa
mara ya kwanza. Mgombea ni Daktari ambae anasema anatengeneza dawa za ukimwi na
ameahidi wapiga kura kutoa dawa yake hiyo bure endapo atachaguliwa.
·
Bibi Edith Z. Nawakwi - Forum For Democracy and
Development (FDD) - ni mgombea pekee mwanamke na mara yake ya tatu
kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Urais.
·
Bw.
Tilyenji Kaunda - United National Independence Party (UNIP)- ni mtoto wa muasisi wa Chama hiki kilichoipatia Jamhuri ya Zambia
uhuru wake kutoka kwa mkoloni, Mhe. Dkt Keneth David Kaunda. Tangu kiondolewe
madarakani 1991, kimeendelea kushiriki kwenye chaguzi hizi bila ya mafanikio ya
kurudi tena madarakani.
·
Brig. Jen. (Rtd) Godfrey Miyanda - Heritage
Party (HP) - anaingia kwenye
kinyang’anyiro kwa mara ya tatu.
·
Bw.
Daniel M. Pule - Christian Democratic Party (CDP)--- anagombea kwa mara ya kwanza.
·
Bw.
Peter C. Sinkamba - Green Party- ni mgombea machachari ambaye anasema akipewa madaraka haya ya juu atafanya
bangi kuwa zao halali la biashara. Ana uhakika kuwa serikali itapata mapato
makubwa kutoka kwenye bangi hivyo kuondoa tegemezi kwenye zao moja tu la shaba.
·
Bw.
Eric M. Chanda – Chama cha 4th Revolution - Chama hiki kinaingia kwenye
uchaguzi wa Rais kwa mara ya kwanza.
Ujumbe
wa Waangalizi kutoka nchi wanachama wa SADC uliopo Lusaka, Zambia akiwemo
Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Grace J. Mujuma umetembelea vituo vya
uchaguzi asubuhi hii na kukuta watu wamejipanga kwenye vituo hivyo tangu majira
ya saa kumi na moja asubuhi.
Kituo
cha kwanza ambacho kilitembelewa na ujumbe huu kilifunguliwa rasmi saa 12
asubuhi kukiwa na wahusika wote na kulingana na taratibu zilivyopangwa na Tume
ya Uchaguzi wa Zambia na uchaguzi kuendelea kwa hali ya shwari.
UBALOZI WA TANZANIA
LUSAKA,
ZAMBIA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...