![]() |
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu |
Wadau wa soka nchini na wateja Vodacom Tanzania kwa ujumla wanaendelea kupata habari za soka zinazohusiana na ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara(VPL)Ligi kuu ya Uingereza,na masuala mengine mengi yanayohusiana ya burudani kupitia simu zao za mkononi kupitia huduma maalum iliyozinduliwa mwaka juzi.
Katika huduma hiyo ambayo inawafanya wateja kupata burudani ili kupata taarifa hizo za michezo na burudani anachotakiwa kufanya mteja ni kutuma neno SPORTS kwenda namba 15778 na hapo mteja atajipatia habari motomoto na burudani kwenye simu yake ya mkononi mahala popote pale aliko.
Akiongea kuhusu huduma hii Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amewasihi wapenzi wa soka na watanzania kwa ujumla kuitumia huduma hii ambapo itawarahisishia kujipatia habari motomoto za michezo na burudani kwa urahisi bila kupoteza muda mwingi.
“Ni rahisi kupata habari za michezo kwa pamoja kupitia simu yako ya mkononi kupitia huduma hii ukiwa popote pale badala ya kupoteza muda mwingi wa kusubiri kusoma magazeti au kufika manyumbani kusikiliza radio na kuzitafuta kwenye intanent,kwa kujiunga na huduma hii utaona maisha yanakuwa murua na tunawaaidi wateja wetu tutaendelea kuboresha huduma zetu na kuwaletea huduma zilizo bora na zenye manufaa kwao”.Alisema Nkurlu.
Vodacom imekuwa ikiboresha huduma mbalimbali ili ziweze kwenda na wakati na kuwanufaisha na kuwapatia burudani wateja wake ambapo mwaka jana ilizindua huduma ya kipekee ya shinda na kabumbu ambayo iliwawezesha wateja wengi kujishindia zawadi za kila aina ikiwemo fedha taslimu.Mbali na huduma kama hizo za michezo Vodacom imekuwa ikiandaa promosheni za kubadilisha maisha ya wateja mojawapo ikiwa ni ile ya Timka na bodaboda na Vodacom milionea ambapo washindi waliweza kujishindia pikipiki na fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 100.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...