Makampuni mengi hapa jijini yamebuni utaratibu wa kuwatumia vijana wanaotembea kwa kutumia viatu vya matairi (Roller Skating) katika kusambaza ujumbe na matangazo yao mbali mbali,jambao hilo ni jema sana hasa ukizingatia kuwa sasa hivi swala la ajira ni changamoto.Vijana hawa hufanya kazi ya kugawa vipeperushi kwa wenye magari na watembea kwa miguu katika makutano makuu wa mabarabara hapa jijii Dar,kama walivyokuta na Kamera Mani wa Globu ya Jamii maeneo ya Magomeni Mapipa hivi karibuni.
Mmoja wa vijana hao akipiga misele barabarani.
Ni vizuri lakini ningeshauri au kupendekeza, vijana hao na hata hao waajiri wao, wazingatie suala zima la 'healthy and safety' kwa vijana hao, hili nikimaanisha uvaaji wa 'High Vis Jackets' ikiwezekana hata helmets, kwani kazi zao hizo na hizo 'roller skating' barabarani ni hatari zaidi na khasa kwa madereva wetu hawa wa kibongobongo wasiojali wala kuzingatia sheria za usalama barabarani, inakuwa ni hatari zaidi endapo hawatavaa reflective and protective equipment wawapo kazini. (Ni ushauri tu)
ReplyDelete