Vyombo
vya habari nchini vimehimizwa kuwasilisha masuala yanayowahusu watoto
yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu. Akizungumza na
wanahabari kutoka vyombo mbalimbali jijini Arusha katika warsha juu ya
HAKI ZA WATOTO YATIMA NA WALE WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
iliyoendeshwa na shirika liliso la kiserikali la The Foundation For
Tomorrow (TFFT).
Mkurugenzi
Mkuu wa Tanzania wa shirika hilo, Bwa. Kennedy Oulu alisema tatizo la
watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu nchini Tanzania ni
gumu, hivyo vyombo vya habari havina budi kuifahamisha jamii kuhusu
hili suala na matatizo yanayowakabili watoto yatima na waishio katika
mazingira magumu ili jamii na wadau mbalimbali waweze kushiriki vema
katika kukabiliana na tatizo hili.
“Kwa
sasa, inakadiriwa kuwa kuna watoto yatima na wale waishio katika
mazingira magumu wapatao 1,800,000 hapa Tanzania pekee, huku 1,300,000
kati yao wakiwa wametokana na athari za ugonjwa wa UKIMWI. Mgawanyo wa
kifamilia na muundo wa kimsaada kijamii ni moja ya vinavyochangia tatizo
hili.
Vinapoongezwa katika umaskini unaojidhihirisha katika: ukosefu wa
upatikanaji wa huduma za elimu ikiwemo elimu ya awali, ukosefu wa
upatikanaji wa huduma za afya na uzalishaji kama afya ya uzazi, ukosefu
wa stadi za maisha zinazoakisiwa katika mitaala ya shule zenye uwezo
unaotakiwa na ubunifu ili kujenga uwezo wa watoto, si kwa yatima na
waishio katika magumu pekee”. Alisema Kennedy na kuongeza.
“Ni
muhimu kutambua kuwa kumekuwa na hatua na mafanikio yaliyofikiwa na
wadau mbalimbali ikiwemo serikali katika kuwezesha upatikanaji,
kuzijengea uwezo familia za watoto hawa na kubadili mitazamo ya jamii
dhidi ya watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu, hii
inajenga msingi wa mwitikio endelevu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...