Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokelewa na baadhi ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya Ziwa na Nishati na Madini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Profesa Muhongo anafanya ziara katika mikoa ya Simiyu, Tabora na Shinyanga lengo likiwa ni kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Taneesco.
Mkazi wa kijiji cha Ihale kilichopo wilayani Busega mkoani Simiyu ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiuliza maswali mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na wananchi (hawapo pichani) mara Waziri alipofanya mazungumzo na wananchi wa kijiji hicho ili kusikiliza kero zao.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo kwenye mkutano na wananchi wa kata ya Ijitu iliyopo wilayani Busega.
Jamani hizo houses kweli zinahitaji umeme?
ReplyDeleteHivi kweli viongozi wetu wanapotembelea sehemu mbali mbali na kukuta makazi ni kama yanavyoonkana hapo huwa wanajiuliza maswali gani akili mwao? Ukizingatia Gari lililompeleka sehemu hiyo ni swa na kujenga kaya tano zenye hadhi ya kukaa binadamu ktk eneo husika.
ReplyDeleteNaomba maoni yako Ankal Michuzi>
Jibu ni yes, as long as they are not built of metal material
ReplyDeleteUmeme hufanya watu kubadili mtazamo wao na hata kujenga nyumba nzuri and vice is true so big up kwa serikali kwa kuwakumbuka watu wa vijijini...
ReplyDeleteProf. Muhongo kwa kuwa umefanikiwa kupenya kwenye Fagio la chuma, sasa jukumu lako ni kuhakikisha bei ya umeme inashuka chini!!!
ReplyDeleteAcha ahadi zako za asali na maziwa tunaaka kazi sasa, ili bei ya umeme ikishuka NI LAZIMA TUTAOPATA MAENDELEO, WANAINCHI WATAISHI MAISHA BORA NA KUWA NA VIPATO HUKU BIASHARA ZIKIINGIZA FAIDA NA NCHI KUFAIDIKA NA KUKUA KWA UCHUMI.
Vijiji venyewe vinaonekana vimechoka kabisa vumbi tupu muhongo kala ela za escrow hajali kabisa
ReplyDelete