Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokelewa na baadhi ya watendaji kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya Ziwa na Nishati na Madini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Profesa Muhongo anafanya ziara katika mikoa ya Simiyu, Tabora na Shinyanga lengo likiwa ni kukagua miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Taneesco.
Mkazi wa kijiji cha Ihale kilichopo wilayani Busega mkoani Simiyu ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiuliza maswali mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na wananchi (hawapo pichani) mara Waziri alipofanya mazungumzo na wananchi wa kijiji hicho ili kusikiliza kero zao.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo kwenye mkutano na wananchi wa kata ya Ijitu iliyopo wilayani Busega.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Jamani hizo houses kweli zinahitaji umeme?

    ReplyDelete
  2. Hivi kweli viongozi wetu wanapotembelea sehemu mbali mbali na kukuta makazi ni kama yanavyoonkana hapo huwa wanajiuliza maswali gani akili mwao? Ukizingatia Gari lililompeleka sehemu hiyo ni swa na kujenga kaya tano zenye hadhi ya kukaa binadamu ktk eneo husika.
    Naomba maoni yako Ankal Michuzi>

    ReplyDelete
  3. Jibu ni yes, as long as they are not built of metal material

    ReplyDelete
  4. Umeme hufanya watu kubadili mtazamo wao na hata kujenga nyumba nzuri and vice is true so big up kwa serikali kwa kuwakumbuka watu wa vijijini...

    ReplyDelete
  5. Prof. Muhongo kwa kuwa umefanikiwa kupenya kwenye Fagio la chuma, sasa jukumu lako ni kuhakikisha bei ya umeme inashuka chini!!!

    Acha ahadi zako za asali na maziwa tunaaka kazi sasa, ili bei ya umeme ikishuka NI LAZIMA TUTAOPATA MAENDELEO, WANAINCHI WATAISHI MAISHA BORA NA KUWA NA VIPATO HUKU BIASHARA ZIKIINGIZA FAIDA NA NCHI KUFAIDIKA NA KUKUA KWA UCHUMI.

    ReplyDelete
  6. Vijiji venyewe vinaonekana vimechoka kabisa vumbi tupu muhongo kala ela za escrow hajali kabisa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...