App inayoonyesha vivutio mbalimbali vya kitalii nchini Tanzania, App hiyo ambayo imeandaliwa na Bi. Benita Cassar Torreggiani kwa kusaidiwa na wataalam kutoka Apple inaweza kupatikana kupitia mitandao ya Ipad, Iphone na Smart Phone.
Mfanyakazi wa Apple Store Grand Centra jijini New York ambako onyesho hilo lilifanyika akimtambulisha Bi. Benita.
Balozi Tuvako Manongi Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akizungumza na Bi . Benita ambapo alimshukuru kwa uamuzi wake huo wa kutangaza utalii wa Tanzania kupitia App hiyo.
Na Mwandishi Maalum, New
York
Katika kuhakikisha kwamba
taarifa kuhusu vivutio
mbalimbali vya kitalii vilivyopo
nchini Tanzania zinawafikia watalii wengi na kwa urahisi
nchini Marekani na kwingineko , jana
( alhamis) palifanyika onyesho la
App inayotoa huduma hiyo kupitia Ipad,
Iphone na Smart Phones.
App hiyo ijulikanayo kama “ Official Destination Tanzania, Zanzibar,
Serengeti, Ngorongoro and Kilimajaro”,
imeandaliwa Bi. Benita Cassar
Tirreggian akisaidiwa na wataalam kutoka kampuni ya Apple kupitia mpango wao
ujulikanao kama one to one.
Onyesho la App hiyo ambalo lilikuwa kivutio kwa wageni walioalikwa akiwamo Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja
wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, limefanyika katika duka linalouza bidhaa za Apple ambalo lipo katika Kituo Kikuu cha Treni ( Grand Central)
jijini New York.
Baadhi ya washiriki kutoka
TANAPA ambao wapo hapa New York kushiriki
onyesho jingine la masuala ya kitalii
maarufu kama New York Times
Travel Show nao walihudhulia onyesho la App hiyo.
Akielezea ni kwa nini
aliamua kutengeneza App hiyo, Bi.
Benita aliwaeleza wageni waalikwa kwamba
mapenzi yake mkubwa kwa Tanzania ndio hasa kulikochangia yeye kuamua kuitengeneza App hiyo ili uzuri wa nchi ya Tanzania, watu wake
na maliasili zake ushuhudiwe na
kuwavutia watu wengi zaidi.
Akaongeza kuwa pamoja na
utaalam na usaidizi kutoka Kampuni ya Apple,
Serikali ya Tanzania pamoja na wadau wa sekta ya utalii, walimpatia
ushirikiano mkubwa katika utengenezaji
wa App hiyo ambayo anasema imeridhiwa na Serikali.
Balozi Tuvako Manongi alimshukuru Bi. Benita kwa uamuzi wake huo na pia
akawashuru wageni mbalimbali waliohudhuria onyesho hilo huku akiwatia shime
ya kwenda Tanzania kujionea na kufurahia
utajiri mkubwa wa maliasili kwa maana ya mbunga za wanyama, bahari yenye kila aina ya vivutio na mengine
mengi ambayo Tanzania imebarikiwa kuwa
nao.
Safi sana-nimesha i download and I can only recommend it :-)
ReplyDelete