Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla ametembelea mamlaka ya maji na usafi wa mazingira mkoani Njombe (NJUWASA) na kutembelea vyanzo vya maji vya Magoda,Hagafilo,Njenga na Kibena pia Amekagua ujenzi wa mradi wa kuboresha maji mji wa Njombe kuanzia kwenye chanzo cha Mto Njenga,ulazaji mabomba na matanki makubwa.

Mradi wa Njenga utagharimu kiasi cha sh. 3.5 bilioni na tayari umeshagharimu sh 2.2 bilioni na utakamilika mapema machi mwaka huu na kuongeza upataikanaji maji kutoka asilimia 43 hadi asilimia 79,Amewataka wakandarasi wote wa mradi huu kukamilisha kazi hiyo mapema mwezi machi ikiwa ni kuanzia chanzo,mabomba na matanki ili wananchi mji Njombe wapate maji ya uhakika.

Aidha amefanya mkutano na wadau wote wa maji mji wa Njombe Naibu waziri akipata maelezo ya chanzo cha maji cha Hagafilo kutoka kwa mdau wamazingira na mlezi wa Walei ndg Edwin kilasi.
Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akielekeza jambo wakati akipatiwa maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji mkoa wa Njombe,Ndg. Daudi Majani.
Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akiangalia uunganishaji na ulazaji wa mabomba maeneo ya airport,kambarage,nzerengerendete na Magereza.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...