Na Bashir Yakub
Mara nyingi nimekuwa nikiandika kuhusu masuala muhimu kuhusu ardhi hasa  namna ya kuandika mikataba  mtu anapokuwa ananunua nyumba/kiwanja , hadhi ya mikataba hiyo kisheria, na ubora wake. 
Pia nimeandika mambo mbalmbali kuhusu namna ya kununua nyumba au kiwanja kwa usalama ili watu wasitapeliwe. Nikasema suala si tu kununua kile unachokipenda na kuondoka isipokuwa ni kununua  na  kuwa salama  na ulichonunua  bila hatari ya kukumbana na mgogoro mbeleni. 
Lengo la haya yote ni katika kuhakikisha watu hawatapeliwi na hivyo kupoteza  fedha walizochuma kwa jasho.Lengo lingine ni kuwaepusha wanunuzi  na hatari ya kuingia mahakamani ambako kuna  usumbufu mkubwa na panapoteza fedha na muda sana tena sana, naongea hili kwa uzoefu. 
Leo pia nasisitiza tena kuwa  ili ununue kiwanja au nyumba  na uepuke kabisa kupata mgogoro hakikisha  unafuata taratibu zote za msingi na za kisheria   ikiwemo kuhakikisha  unaandaa mkataba wenye hadhi  ambao  hata likitokea tatizo basi mkataba uwe ndio mlinzi wako.  Aidha leo naongelea tatizo lingine tena katika  masuala hayahaya ya  manunuzi ya viwanja na nyumba. Naongelea fedha ambayo serikali za mitaa wamekuwa wakiichukua kutoka kwa watu wanaouziana  ardhi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Dah ahsante kwa kunijuza...Me nilikuwa sijui kuwa haiko katika sheria !! Dahhh walinisumbua sana hawa....Ngooja now nimeshafumbua macho

    ReplyDelete
  2. Wewe mwanasheria, usije ukatuingiza mkenge, tukanunua nyumba, viwanja, halafu vikawa na migogoro, aidhi vimeuzwa mara kumi, halafu wewe unasema sio lazima kupitia serikali za mitaa, wakati serikali za mitaa ndio wahusika/wenyeji wa maeneo hayo. hebu tueleweshe vizuri mwanasheria. mimi nilikwenda kununua kiwanja yombo vituka, kumbe huyo mwenye kiwanja alikuwa tapeli, kilichoniokoa ni serikali za mitaa, na nikawa nimeokoa pesa yangu. sasa kama kweli sharia ndivyo inavyosema, nina mashaka kidogo. pia juzi nilinunua shamba hekali kumi, bila kupitia serikali ya mitaa, kumbe wauzaji walikuwa ni walinzi wa eneo hilo, na mara baada ya muda tukakamatwa kama wavamizi wa shamba hilo. kwa kweli ingekuwa tumepitia kwenye serikali ya mtaa tusingepata shida hiyo. hapo unasemaje?

    ReplyDelete
  3. TWILA KAMBANGWAJanuary 15, 2015

    mwanasheria asante sana klwa hili na asante kwa kutujuza kaka

    ReplyDelete
  4. Asante sana kwa kuelimisha umma katika masswala ya ununuzi na uuzaji wa ardhi na nyumba. Watanzania tunahitaji elimu, na elimu tu ndio itatukomboa. Inasikitisha sana kuona kwamba rushwa imekuwa kama ni kiungo cha muundo wa serikali ya Tanzania.

    ReplyDelete
  5. je ? ukitaka ku repair nyumba,kama kubadilisha bati au ukuta umeanguka ni lazima kuomba kibari serikali za mitaa au kuwausisha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...