Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitka kutangaza kuwa treni za abiria za kwenda Kigoma hazitofika katika stesheni ya Kigoma badala yake zitatumia kituo kidogo cha Katosho.
Kwa mujibu wa wa taarifa ya Uongozi wa TRL lilitolewa Februari 16, 2015 uamuzi wa treni kutofika katika stesheni ya Kigoma unatokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mjini Kigoma na hivyo kuzoa mchanga ambao umefunika tuta la reli katika eneo la stesheni ya Kigoma.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo abiria wote wanaowasili na wale wanaondoka Kigoma itawalazimu kujitegemea usafiri kwenda makwao na pia wale watakaosafiri kuja Tabora na Dar es Salaam kwa kutumia kituo kidogo cha Katosho.
Mara baada ya hali kutengemaa na kurekebishwa miundo mbinu ya reli katika stesheni ya Kigoma huduma zitarejeshwa kama kawaida.
Aidha Uongozi wa TRL unawaomba radhi wateja wake na wananchi kwa jumla hasa wa mkoa wa Kigoma kwa usUmbufu utakajiotekeza .
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji ,
Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
Dar es Salaam,
Februari 18, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...