Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akiwafafanulia jambo maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama
ya nchini Marekani katika mkutano wao uliofanyika jijini Washington DC katika Ukumbi wa Mkutano wa Ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani. Katika mazungumzo yao maafisa hao wa Marekani wanatarajia kutua nchini Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa maafisa
Uhamiaji, Polisi na Maafisa Forodha ya kushirikiana kwa Serikali hizo mbili kwa ajili ya kudhibiti mipaka kwa kuzuia bidhaa haramu zikwemo
silaha, dawa za kulevya pamoja na bidhaa mbalimbali za hatari kwa maendeleo ya nchi ambazo zinaweza kuingizwa nchini kutoka kwenye nchi
mbalimbali duniani. Waziri Chikawe yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi
duniani hata hivyo alipata muda wa kuzungumza na maafisa hao baada ya kuomba kukutana naye. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini
Marekani na Mexico, Liberata Mulamula.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wanne kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula
(watatu kushoto), na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, jijini New York, nchini Marekani, Tuvako Manongi
wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani pamoja na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani na
Usalama ya nchini Marekani. Waziri Chikawe alikutana na Maafisa hao wa Marekani, jijini Washington DC kujadiliana masuala mbalimbali
likiwemo la Maafisa hao wakitarajia kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa maafisa Uhamiaji, Polisi na Maafisa Forodha ya
kushirikiana kwa Serikali hizo mbili kwa ajili ya kudhibiti mipaka kwa kuzuia bidhaa haramu zikwemo silaha, dawa za kulevya pamoja na bidhaa
mbalimbali za hatari kwa maendeleo ya nchi ambazo zinaweza kuingizwa nchini kutoka kwenye nchi mbalimbali duniani. Waziri Chikawe yupo
jijini Washington DC katika Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani, hata hivyo alipata muda wa kuzungumza na
maafisa hao baada ya kuomba kukutana naye. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati) akimsalimia Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, jijini New York, nchini Marekani, Tuvako Manongi wakati Waziri huyo alipowasili ubalozi wa Tanzania nchini humo uliopo katika Jiji la Washington DC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati), Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Liberata Mulamula (kushoto) na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, jijini New York, nchini humo, Tuvako Manongi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumpokea Waziri huyo aliyewasili jijini Washington DC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kupambana na Vurugu na Ugaidi duniani unaotarajiwa kufanyika jijini humo kesho.Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...