Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akimshukuru mwakilishi wa kampuni ya utalii ya Escape Bwana Nassri Chaouki baada ya kutembelea banda la kampuni hiyo inayoshiriki Maonesho ya Utalii ya Brussels. Balozi Kamala aliishukuru kampuni hiyo kwa kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania.
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kushoto) akimsikiliza mwakilishi wa kampuni ya utalii ya Terre D'Afrique ya Brussels inayotangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana Tanzania. Balozi Kamala ameishukuru kampuni hiyo kwa kutangaza vizuri Tanzania katika Maonesho ya Utalii yanayoendelea jijini Brussels.
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala P AKIWA katika picha ya pamoja na Bwana Burt Munting Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Habari Travel ya Uganda inayoshiriki Maonesho ya Utalii ya Brussels. Balozi Kamala ameishukuru kampuni hiyo kwa kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana Tanzania.
Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala P akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Masoko wa kampuni ya kutangaza utalii ya Travel Xenarjo ya Ubeligiji Bi. Dana Maes baada ya kutembelea Banda la kampuni hiyo inayoshiriki Maonesho ya Utalii ya Brussels. Kampuni hiyo imekubali kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana Tanzania baada ya Balozi Kamala kuiomba kampuni hiyo kufanya hivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...