Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Bwana Jorge Luis Lopez alisema kwamga upo umuhimu mkubwa wa kuwa na mabadiliko ya mafungamano ya uhusiano wa Kiuchumi na kisiasa kati ya Taifa lake na Marekani. Alisema mafungamano hayo ambayo hayakuwepo kati ya Mataifa hayo ya Bara la America ya Kusini kwa takriban miaka 50 iliyopita endapo yataimarishwa vyema yanaweza kusaidia ustawisha kizazi cha sasa na hatma ya kizazi kijacho.

Balozi huyo wa Cuba Nchini Tanzania Bwana Jorge Luis Lopez alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Akitoa ufafanuzi kufuatia Kikao cha hivi karibuni cha mafungamano kati ya Rais Raul Castro wa Jamuhuri ya Cuba na Rais Barak Obama wa Marekani Balozi Lopez alisema yapo mambo mengi ya msingi ambayo pande hizo mbili zitalazimika kuyakalia pamoja kwa lengo la kuyashughulikia kwa kina.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema kwamba mafungamano hayo ya Marekani na Cuba ni Habari njema inayotoa matumaini mapya ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili ambayo haukuwepo kwa nusu Karne iliyopita.

Balozi Seif alisema iwapo nia ya Rais Raul Castro wa Jamuhuri ya Cuba na Rais Barak Obama wa Marekani itakuwa sahihi kuna fursa pana ya kujenga na kuimarisha uchumi baina ya Mataifa hayo Mawili ambapo pia Cuba inaweza kuitumia nafasi hiyo kwa kujitangaza na hatimaye kujitanua kiuchumi katika pembe zote za Dunia.
Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Bwana Jorge Luis Lopez akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwa Mhe. Makamu Vuga Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa pili kutoka kulia akizaungumza na Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Bwana Jorge Luis Lopez aliyepo kulia yake hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Katibu Wake Bwana Abdulla Ali Abdulla { Kitole } na kulia ya Balozi Lopezi ni Ofisa wa Idara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Zanzibar Bwana Iddi Seif Bakari.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo wa Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini Tanzania Bwana Jorge Luis Lopez aliyefika Ofisini kwake Vuga kusalimiana naye. Picha na – OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...