NA BASHIR YAKUB-
Upo wakati kwenye ndoa ambapo mmoja wanandoa anaweza akawa anataka kuuza au kubadili jina la nyumba/kiwanja bila ridhaa ya mwenzake ilihali nyumba hiyo ni ya familia. Lakini pia nje ya hilo kuna mazingira ambayo mtu anaweza kuwa si mwanandoa lakini ana maslahi katika nyumba au kiwanja cha mtu fulani na anataka kuzuia nyumba/ kiwanja hicho kisibadilishwe jina au kisiuzwe. Kisheria jambo hilo linaruhusiwa na huitwa zuio( Caveat).
Hili sio zuio la kwenda mahakamani kama mazuio tuliyoyazoea.Hili ni zuio jingine kama nitakavyolieleza. Aidha kuzuia hati isibadilishwe kimsingi ni sawa na kuzuia nyumba isiuzwe. Hii ni kwakuwa hakuna namna ambavyo mnunuzi anaweza kununua kitu ambacho hakiwezi kubadilika na kuingia katika jina lake. Ikiwa mke ana wasiwasi kuwa mume anaweza kumzunguka na kuuza mali ya familia au mume ana wasi wasi juu ya uwezekano wa mke kuuza basi wanayo ruhusa ya kuweka zuio ili hati ya nyumba isibadilishwe. Yapo mambo mengi kuhusu hili nitaeleza baadhi.
1. NINI MAANA YA ZUIO.
Zuio ni usitishwaji wa muda ambao huwekwa ili kuzuia mabadiliko yoyote katika hati. Kama maana yenyewe inavyojieleza huu unakuwa ni usitishwaji wa muda ambao unalenga kulinda maslahi ya mtu aliyeomba zuio.Kuitwa zuio la muda haimaanishi kuwa mtu akizuia itakuwa ni mwezi mmoja au miwili basi, hapana. Ni zuio la muda kwakuwa haliwezi kukaa milele lakini mtu akishaliweka linaweza kukaa hata miaka mingi kutegemea na sababu za zuio hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...