DSC_0003
Balozi wa India nchini, Mh. Debnath Shaw akisalimiana na Daktari bingwa wa Afya ya jamii na familia, Dkt. Ali Mzige kwenye hafla fupi ya kukabidhi madawati 50 pamoja majengo mawili ya shule ya msingi Kibugumo yaliyokarabatiwa na umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO. Katikati ni Mbunge wa Kigamboni Dk Faustine Ndungulile. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi wetu

WANAFUNZI 150 waliokuwa katika dhiki ya elimu shule ya msingi Kibugumo kutokana na kulazimika kusoma wakiwa wameketi sakafuni wamekabidhiwa madawati yatakayowawezesha kusoma kwa raha.

Madawati hayo yamekabidhiwa jana na umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO mbele ya shuhuda ya balozi wa India nchini, Debnath shaw.
Pamoja na madawati hayo taasisi hiyo ilikabidhiwa madarasa mawili yaliyokarabatiwa.

Akipokea msaada huo Kaimu Ofisa elimu wa Manispaa ya Temeke Angelina Nasazwa, alisema umekuja wakati muafaka hasa kwa kuangalia changamoto nyingi zilizopo katika shule hiyo, ikiwemo miundombinu ya madarasa na ofisi.
DSC_0026
Balozi wa India nchini, Mh. Debnath Shaw (wa pili kulia) akiteta jambo na Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile (kulia) kwenye hafla fupi ya kukabidhi madawati 50 pamoja majengo mawili ya shule ya msingi Kibugumo yaliyokarabatiwa na umoja wa jamii ya watu kutoka India Bengali waliopo hapa Tanzania, BANGO SANGHO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...