Sehemu ya Ghala la kuhifadhi vitunguu Saumu liliojengwa na MIVARF, lipo Mkoani Manyara Wilayani Mbulu, kijijini Bashay. Ghala hilo lina uwezo wa kuhifadhi tani 50 za vitunguu Saumu.
Na. Ibrahim Hamidu
Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za
Kifedha Vijijini (MIVARF) imeboresha Soko la Vitunguu Saumu kwa kujenga
ghala la kuhifadhi vitunguu mkoani Manyara, wilayani Mbulu katika kijiji
cha Bashay.
Ghala hilo lenye uwezo wa kuhifadhi tani 50 za vitunguu, limegharimu
Jumla ya shilingi milioni 88 ikiwa MIVARF imechangia asilimia 95 ya fedha
hizo na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imechangia asilimia 5 ya fedha
hizo.
Akiongea na timu ya wataalam kutoka MIVARF ofisini kwake hivi karibuni
wakati timu hiyo ilipokuwa ikikagua utekelezaji wa shughuli za Mradi huo,
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Nicholaus
Haraba, alifafanua kuwa ujenzi wa ghala hilo umeongeza mnyororo wa
thamani wa zao la vitunguu Wilayani Mbulu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...