BENKI ya Exim imetoa
wito kwa wateja wake kutumia vyema fursa ya ugunduzi uliopo katika sekta ya
gesi nchini kwani ina uwezo
wa kubadilisha muundo wa uchumi uliopo na kujenga uchumi mpya uliojengeka
katika utegemezi wa gesi asilia ambao utakua na matunda makubwa katika sekta
mbalimbali ikiwemo sekta ya kibenki na biashara.
Wito huo ulitolewa na
Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa benki hiyo, Bw. Dinesh Arora wakati wa hafla fupi
iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni maalum kwa ajili
ya wateja wake wakubwa.
Zaidi ya hayo, Arora alieleza
kuwa sekta ya gesi inaambatana na fursa nyingi
ambazo zinaweza kutumiwa na wadau mbali mbali waliopo katika sekta
binafsi. Alitaja maeneo yenye fursa kuwa ni pamoja na matengenezo ya
vifaa, ujenzi, huduma za mazingira
na Mafunzo ya Ufundi.
“Ni imani yetu kama
benki ya Exim kuwa, katika siku zijazo, kutakuwa na ongezeko kubwa la mahitaji
ya makazi, sehemu za burudani, utalii, elimu na huduma za afya. Jukumu kubwa la
sekta binafsi itakuwa ni kukuza uhusiano na sekta ya gesi na kugundua na
kuzitumia fursa,” alisema.
Akizungumzia juu ya ukuaji
wa uchumi nchini, Arora alisema kuwa makampuni yanahitaji mipango na mikakati
ya kifedha ya muda mrefu ili kuweza kufikia mahitaji na malengo yao ya ukuaji.
“Kama benki ya
tano kwa ukubwa Tanzania, Benki ya Exim inatoa huduma za kibenki za uwekezaji
katika mfumo wa ushauri na ‘intermediary’ ili kuzalisha na kuongeza mtaji kwa
njia ya ‘debt and equity’ kwa wateja wakubwa,” alisisitiza..
Arora aliendelea kuwaasa
wateja kutumia kitengo cha benki hiyo cha huduma za kibenki za uwekezaji,
ambacho kwa sasa kina huduma mpya zilizotengenezwa maalum ili kukidhi mahitaji
mahsusi ya wateja wake, zikiwemo Project Financing, Debt na Equity Syndication
services na Private Equity na M & A Advisory Services.
Arora alisema kuwa benki
yake imejenga uwezo mzuri kati ka
suala hilo na
piaimeongeza nguvu zaidi
katika muundo wake wa
uongozi ili kusaidia katika kurahisisha uwepo wa uhusiano wa
kimataifa na kuongeza mtandao na
wawekezaji. “Tumejiimarisha zaidi na tumefanya maombi ya vibali mbalimbali
stahiki na pia tumeungana na wawekezaji,” alisema.
Akizungumzia huduma zinazopatikana katika kitengo hicho
cha huduma za kibenki za uwekezaji, Arora alisema
moja ya huduma zinazotolewa na kitengo hicho ni pamoja na ushauri bora wa
kimkakati kwa wateja wake.
“Muundo wa benki yetu
unaturuhusu kuwahudumia wateja wetu na kuwapatia ufumbuzi wa mahitaji yao ya
kimkakati na kifedha katika nyanja zote. Tunawiwa kuwa mshauri nambari moja kwa
wateja wetu ikiwa ni pamoja na makampuni binafsi, taasisi za fedha, mamlaka za
umma, wawekezaji na wakopeshaji,” alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...