NA BASHIR NKOROMO.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema, hakuna kitakayempitisha kugombea urais 2015, kwa presha za makundi au wapambe.
Akizungumza
kwa nyakati tofauti katika vyumba vya habari vya magazeti ya Habari
Corporation, na Mwananchi Communication Ltd, jijini Dar es Salaam, leo,
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, mfumo wa CCM
katika kuwapata wagombea ni imara kiasi kwamba hautaweza kuathiriwa na
presha za makundi wakati wa kuteua mgombea urais katika uchaguzi mkuu
mwaka huu.
Amesema,
ni vigezo vinavyozingatia kanuni na katiba ya Chama tu ndivyo
vitakavyomuwezesha anayetaka kupeperusha bendera ya CCM kupitishwa na
Chama, vinginevyo haitawezekana hata kama ana makundi yenye presha kiasi
gani.
"Chama
hiki kina mfumo na taratibu ambazo haziwezi kusukumwa na presha za
wapambe wa mgombea yeyote, na hata kumbukumbu zinaonyesha kwamba katika
chaguzi zilizopita, wamewahi kuwepo wagombea wenye makundi yenye presha
kiasi cha kudhaniwa ndio wangeteuliwa, lakini baada ya kufika mbele ya
taratibu na kanuni waliachwa na nafasi kupewa wengine", alisema Nape.
Alisema,
kanuni na taratibu ndizo mwamuzi wa mwisho katika kuteua wagombea wa
CCM, "Sisi tukisema wanaotaka nafasi hii njooni mjipime hapa, mmojawapo
akijaiona hatoshi lakini kwa ujanja akaongeza matofali kupata urefu...
huyo taratibu zitatumia kuondoa matofali ili abaki kama alivyo kuona
kama anatosha", alisema Nape.
"Na katika utaratibu huu wa kuondoa matofali ndiyo watajitokeza baadhi yao kulalamika kwa sababu itauma kidogo", alisema.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...