Mkurugenzi Mkuu wa VIVA Tower Viral Manek, akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya I&M katika jengo hilo litakalotoa huduma masaa 24, kwa kuweka na kutoa fedha na kubadilisha fedha za kigeni kwa kutumia mfumo mpya wa mashine za kieletroniki (ATMs). Kushoto ni mkurugenzi mkuu wa benki hiyo, Bw. Anurag Doreha, Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya I&M, Anurag Doreha (katikati) akifafanua jambo baada ya uzinduzi wa tawi jipya la benki hiyo kufanyika katika jengo la Viva Tower ambapo huduma za kuweka, kutoa na kubadilisha fedha za kigeni zitakua zikifanyika masaa 24 kutumia mashine za kielektroniki(ATMs) kulia ni Mkurugenzi mkuu wa VIVA Tower Viral Manek na kushoto ni Meneja Masoko wa Smart Banking Solutions Limited, Salil Abbas Sadik. Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika Viva Tower-Posta jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mkuu wa VIVA Tower Viral Manek, akionesha kwa vitendo jinsi ya kuweka fedha katika moja ya mashine za kielektroniki ndani ya tawi jipya lililozinduliwa la benki ya I&M ikishirikiana na Smart Banking Solutions-Viva Tower-Posta jijini Dar es salaam ambapo mteja anaweza kuweka na kutoa fedha masaa 24 sambamba na kupata huduma ya kubadilisha fedha za kigeni kwa kutumia mashine za kielektroniki(ATMs).
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya I&M, Anurag Doreha akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya mashine inayotumika kubadili fedha za kigeni, baada ya kuzindua tawi jipya la benki hiyo maalum kwa shughuli za kuweka na kutoa fedha kwa kutumia mfumo mpya wa kielektroniki kupitia mashine za (ATMs). Hafla hiyo ilifanyika katika jengo la Viva Tower-Posta jijini Dar es Salaam ambapo benki hiyo imeshirikiana na kampuni ya Smart Banking Solutions Ltd.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. ASANTE SANA I&M NA BARCLAY'S BANK KWA KUANZISHA CASH DEPOSIT MACHINE SASA WALE BANK TELLERS WANAOJIFANYA KAMA BANK ZA BABA YAO BADALA YA KUTOA HUDUMA WAKO BUSY NA SIMU KERO HII IMEONDOKA

    CHANGAMOTO KWA SOKO LA AJIRA NCHINI BANK NYINGI WAMEAJIRI HAWA SO CALLED BANK TELLERS NA HUA WANARINGA SANA KWA KUSHIKA HELA WAKIDHANI NI ZA KWAO ILA SASA CHA MOTO WATA KIPATA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...