Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi imeendesha mafunzo kwa walimu ,wataalam wanaosimamia wanafunzi wa fani ya ununuzi na ugavi wanaofanya tafiti kama sehemu ya mafunzo yao ya stashahada ya ununuzi na ugavi. 

Mafunzo hayo yalifunguliwa jana, na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi, Bw, Aziz Kilonge, ambaye aliwaasa wataalam hao kuhakikisha kwamba wanasimamia wanafunzi kwa ukamilifu ili kuongeza ubora wa kazi za utafiti zinazofanywa. 

Aidha, alifafanua kuwa uzingatiaji wa maadili katika kufanya tafiti, ndio msingi na matakwa ya Bodi, ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanafanya tafiti na sio kuchukua kazi zilizofanywa na wanafunzi/watafiti wengine au kufanyiwa na watu wengine. Pamoja na kuwajengea uwezo wa kufanya tafiti, pia wanafunzi wanajengewa uwezo wa kuandika ripoti na hata kuwasilisha ripoti katika sehemu zao za kazi. 

Hivyo lengo kuu ni kuwejengea uwezo wa kutoa huduma bora kwa taifa. Aliwakumbusha wasimamizi hao kuwajengea wanafunzi hao uwezo wa kujiamini na kujieleza kwani ufaulu wa mwanafunzi, unategemea sana uwezo wake wa kuitetea kazi yake, ambapo katika mtihani huo mwanafunzi atawasilisha kazi yake mbele ya wataalam, ili kupima uwezo wake.
1
Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya PSPTB, Bw, Aziz Kilonge akifungua mafunzo ya Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwa kutoa mafunzo kwa walimu ,wataalam wanaosimamia wanafunzi wa fani ya ununuzi na ugavi wanaofanya tafiti kama sehemu ya mafunzo yao ya stashahada ya ununuzi na ugavi mafunzo hayo yamefanyika kaktika ukumbi baraza la Maaskofu TEC jijini Dar es salaam.
02Tesha Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Dr Clemence akizungumza katika mafunzo hayo mara baada ya kufunguliwa rasmi. 

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...