Na Chalila Kibuda.
MOTO umezuka mapema leo na kuteketeza majengo matatu ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika makutano ya Mtaa wa Libya na Mosque jijini Dar es Salaam.
Moto huo ulioanza majira ya saa tatu asubuhi kwa kuanza kufuka moshi na baadae kuwaka na kuteketeza eneo lote la juu ya majengo hayo.
Akizungumza leo na waandishi wa habari katika eneo la tukio Kamanda wa Kanda Polisi Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova amesema vikosi vya uokoaji na Zimamoto vimefanya ushirikiano katika kuzima moto huo baadhi ya maeneo na kuokoa maduka katika majengo hayo.
‘’Vikosi vya zimamoto vimefanya ushirikiano kwa kuleta magari sita ya kuzima moto na kufanikisha kuuzima moto ambao ulikuwa mkubwa sana’’amesema Kova.
Kova amesema kuwa vikosi vya ukoaji vya zima moto vimefanya kazi kwa ushirikiano ambavyo ni Zimamoto za Uwanja wa Ndege,Zimamoto ya Kampuni ya Ulinzi ya Ultimate,Night Support ,pamoja na Kikosi cha Zimamoto ya Jiji.
Amesema kuwa chanzo cha moto bado hakijafahamika mpaka sasa na uchunguzi wa kubaini chanzo cha moto huo bado unaendelea.
Naye Kamishna msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Kanda Maalum ya Dar es salaam,Jeswald Nkongo amewataka wananchi kutoa taarifa mapema pindi waonapo matukio ya moto na sio kudharau kwa kuamini kuwa moto ni mdogo na wanaweza kuudhibiti.
Moto Mkubwa umezuka mapema leo kwenye moja ya nyumba pichani iliopo mtaa wa Libya na Mosque jijini Dar es salaam na kuteketeza mali kadhaa. Kikosi Kazi cha Globu ya Jamii kipo eneo la tukio kwa sasa kikiendelea kukusanya kila kinachojiri,lakini kwa taarifa kutoka kwa mashuhuda waliopo eneo la tukio wanaeleza kuwa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika rasmi,Jeshi la Polisi limefika eneo la tukio kuhakikisha amani na utulivu vinakuwepo huku magari ya zimamoto nayo yakiendelea kuwasili kupambana na moto huo..
Mmoja wa wapiga picha akitazama kwa mshangao moto mkubwa uliokuwa ukiendelea kuwaka kwa nguvu na kuteketeza baadhi ya mali zilizomo ndani ya jengo hilo lililopo mtaa wa Libya na Moski-Kariakoo jijini Dar.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Kamanda wa Polisi Kanda Maalim ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova akizungumza na vyombo vya habari.
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Jeswad Nkongo akizungumza na vyombo vya habari juu ya walivyofanikiwa kuudhibiti moto huo.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI NA HAMIS MAKUKA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...