Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mimi nimekulia jijini Dar miaka ya 1970, 1980 na 1990 na ajali za moto katikati ja jiji la Dar-es-Salaam ilikuwa ni nadra kuisikia au kutokea.

    Na kama ajali ya moto ikitokea vifaa vya mwanzo vya kuzima moto kama mitugi ya gesi aina ya foam, carbonCo2 ilikuwepo mingi kwenye majengo ya ghorofa hizo ndogo za NHC, majumba ya taasisi za serikali na hata ktk shule mbalimbali zilizokuwepo ktk jiji la Dar iliyokuwa ndogo.

    Na pia kituo cha Fire eneo la Fire jijini DSM walikuwa wana nyezo kama magari na mabomba maalum barabarani ya kujaza maji magari ya zimamoto.

    Swali kuu ni kuwa, je baada ya jiji la DSM kupanuka mno na kuwa kubwa miundo mbinu ya kukabiliana na ajali za moto pia imepanuliwa na kuboreshwa?

    Pia kuhusu vifaa vya mwanzo kukabiliana na ajali ya moto majumbani, maofisini, mashuleni, masoko n.k kama mitungi ya foam, Carbon Co2 kabla magari ya zimamoto hayajafika ktk eneo la ajali ya moto vipo? Pia wenye nyumba, majumba, maofisi na taasisi mbalimbali wana mafunzo ya kukabiliana na moto kwa kutumia vifaa vya mwanzo?

    Pia sheria ndogo ndogo kama za halmashauri za wilaya, serikali za mitaa zipo? Ili kuhakikisha wananchi wana vifaa vya mwanzo vya kukabiliana na ajali ya moto kabla magari ya zimamoto hayajawasilia ktk eneo husika?

    Mdau
    Mtoto wa Mujijini
    Diaspora

    ReplyDelete
  2. Hongereni wananchi kushirikiana na zima moto kwa kuudhibiti moto huo ambao haujaleta madhara ya kibinadamu. Mali kama mali zitapatikana tu kubwa ni kwamba hakuna athari ya binadamu. Watumiaji wa umeme tuwe makini katika utumiaji wa umeme na pia kujenga kasumba ya kuita Tanesco kufanya uchunguzi majumbani mwetu hasa kuona na kubadilisha nyaya za umeme zilizochoka.

    ReplyDelete
  3. Moto utaendelea kutuathiri waTz iwapo hatubadiliki kitaifa.Faya haina magari,vitendea kazi,wala askari wa kutosha.Pia hamna njia wala anuani za kueleweka.Mwisho sote tuwe na ustaarabu wa kupisha magari ya ving'ora.Kitaifa tunahitaji kuwekeza kifedha na kielimu;sio blabla.

    C,mzee wa Ukonga

    ReplyDelete
  4. Jamani hivi vifaa feki vya china vya umeme mbona vitatumaliza. Ndio vinavyosababisha hii mioto yote. Mungu tunusuru na hili janga.

    ReplyDelete
  5. Ushajua faya haina magari. Wakiitwa wanachelewa. Wakija hawana maji. Nyumba yk thamani milioni 20. Ukizungusha raundi elfu 50. Kununua fire extinguisher ya nyumbani hutaki. Bima huna. Unalalamika bila kuchukua hatua

    ReplyDelete
  6. Tanesco wanaozima na kuwasha umeme kama wanacheza gemu wao ndio wanahatarusha maisha ya watu kizaidi na misiba haiishi.

    ReplyDelete
  7. TWILA KAMBANGWAFebruary 11, 2015

    mungu awanusuru vp wakati hamna vifaa vya kuzimia moto? sio kila siku mungu, mungu ndiyo aliyoleta umeme?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...