TIMU ya Coastal Union ya Tanga imesema kuwa itapambana vilivyo ili kuweza kuhakikisha inachukua pointi tatu muhimu dhidi ya Mbeya City kwenye mechi ya Ligi kuu soka Tanzania Bara itakayochezwa wikiendi hii kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani,jijini Tanga.

Coastal Union itangia kwenye mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mechi yao ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa sokoine jijini Mbeya ambapo Mbeya City iliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ambalo lilipatikana kwa njia ya penati.

Akizungumza maandalizi ya kuelekea mchezo huo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga alisema kuwa maandalizi ya kuelekea mechi hiyo imekamilika kwa asilimia kubwa kwa kufanya mazoezi asubuhi na jioni.

Amesema kuwa mipango yake mikubwa ni kuhakikisha wanafuta machungu ya kufungwa na Yanga bao 1-0, kwenye mechi yao ya Ligi kuu iliyochezwa kwenye uwanja wao wa nyumbani jambo ambalo halikuwafurahisha mashabiki na wapenzi wa soka.

Aidha amesema kutokana na kikosi chake kuendelea kuimarika kila mchezo wanaokuwa wakicheza wana matumaini makubwa ya kupata ushindi ambao utawawezesha kusogea kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi hiyo.

Alisema kuwa ligi kuu msimu huu imekuwa ni ngumu sana lakini kubwa ni kujipanga hivyo wamejipanga vizuri kwa umakini mkubwa lengo likiwa kukiwezesha kikosi hicho kinapata matokeo mazuri

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hivi Mbeya City hamnaga jezi za rangi nyingine? au do utaratibu wa mpira hata tu kubadili rangi basi inapendeza.

    ReplyDelete
  2. Mbeya Kaza Butu Kama La Mecco na Tukuyu

    ReplyDelete
  3. Mbeya city aaaall day baby!! Shoot down those wagosi wakaya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...