Mmoja wa waasisi na viongozi wakongwe wa CCM Hajat Kijakazi Salum Kyerula amefairiki dunia  jijini Dar es salaam jana. Taratibu za mazishi  zinafanyika mikocheni eneo la Victoria karibu na Oil com pamoja na hospitali ya Kairuki,  jijini Dar es salaam. Swala ya maiti itafanyika hapo hapo Mikocheni sambamba na swala ya Ijumaa na baadaye  maziko yatafanyika Mtoni Kijichi, kwenye makaburi ya  njia panda ya Neruka.

WASIFU WA MAREHEMU
HAJAT KIJAKAZI SALUM KYELULA NA RATIBA YA MAZISHI

Hajat  KIJAKAZI SALUM KYELULA alizaliwa tarehe 1/1/1941, katika uhai wake amefanya kazi Radio Tanzania(TBC),  Shirika la Habari la Tanzania (SHIHATA).  PIA  Marehemu kijakazi amewahi kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)  Wilaya ya Ilala. katibu mkuu wa CCM mkoa wa Morogoro na Kilimanjaro kwa vipindi tofauti.
 Marehemu amekuwa Mbunge wa Taifa kwa takribani miaka 15,  Naibu Waziri  Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto, Pamoja na nafasi hizo Bi. Kijakazi ni mwanzilishi wa umoja wa  kina mama wa Regent (Regent Women Neighbourhood -  REWONE),  umoja wa kina mama wa kiislamu MIKOCHENI(SAFINA), na pia alikuwa ni mmoja wa waanzilishi wa msikiti wa Regent Estate.
Marehemu ameacha watoto 7 ,wajukuu 14 na vitukuu viwili.
Innalilah wainailalai Rajiun

                                  RATIBA YA MAZISHI  LEO MTONI KIJICHI, DAR ES SALAAM                                                           
                 TUKIO
                 MUDA   
             MUHUSIKA
KISOMO(SURAT RAHMAN & SURAT YASSIN)
SAA 5:00 ASUBUHI
ABDALLAH KIONGA
WASIFU WA MAREHEMU
SAA 5:50 ASUBUHI
RAMADHANI KITWANA
SADAKA
SAA 6:OO MCHANA

KUELEKEA MSIKITINI KWA SALAT JUMAA NA SALAT JANAIZA
SAA 6:45 MCHANA
ABDALLAH KIONGA
MSAFARA KUELEKEA MTONI KIJICHI
SAA 7:15 MCHANA
MJOMBA MSAKUZI
MSAFARA KUFIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU KIJICHI KWA SALAT JANAIZA NA KISHA KUELEKEA MALALONI
SAA 8:15 MCHANA
MJOMBA HAJJI






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Innalillah wajnarajuun...

    Mwenyezi mungu amjaalie amfanyie wepesi katika safari yake hii na amsamehe makosa yake amin

    na ampe kauli dhabit hakika sisi binaadam kwa allah ndio marejeo yetu

    na wafiwa poleni sana allah atawapeni nguvu katika kipindi hichi kizito sana kwenu...amin

    ReplyDelete
  2. Inna Lillahi Wainna Ilayhi Rajiuna. Mwenyeez Mungu akulaze pema peponi Bi Kijakazi Salum Kyerula - Ameen. Akughufirie kwa yote, akunusuru na adhabuze zote za dunia, za kaburi na za kesho akhera. Akupumzishe katika kivuli chake na kesho uwe ni miongoni mwa waja wake wema watakaoingia katika yaje Jannatu N'naeem. In Sha Allah - AMEEN.

    Poleni ndugu, jamaa na marafiki wote mliofikwa na kuguswa na msiba huu. Poleni sana.

    ReplyDelete
  3. Innaa lillaahi wainnaa ilayhi raajiun.Allahumaghfirlahaa waaskinha fil jannati.haya mambo ya uzushi uzushi ya visomo,sijui ratiba tuachane nayo jamani.tufate sunnah ya mjumbe wa Allah

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...