Licha ya jitihada zinazoendelea kufanywa kuzuia uhujumu miundombinu ya Majisafi na wizi wa Maji,
hujuma nyingine kubwa ya chuma chakavu za MAJITAKA imebainika baada ya DAWASCO kukamata
mifuniko ya Majitaka katika kiwanda cha nondo cha IRON&STEEL cha jijini Dar es salaam.
Vyuma Chakavu hivyo ambavyo ni mifuniko ya chemba za Majitaka za DAWASCO zimebainika baada ya
uchunguzi wa kina na taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuhusu upatikanaji wa mifuniko hiyo kiwandani
hapo.
Afisa Uhusiano wa DAWASCO Bi Everlasting Lyaro alisema ilibidi watumie mbinu mbadala ili kubaini
biashara hiyo iliyokuwa ikiendelea kiwandani hapo, ambapo kwa kushirikiana na Polisi kutoka kituo cha
kijitonyama na Afisa Mtendaji wa kata ya Mikocheni waliweza kuvamia kiwanda hicho na kukuta mifuniko
mingi ya chemba za Majitaka ambazo ni mali ya DAWASCO.
“Bei ya mfuniko mmoja wa Majitaka huwa tunanunua kati ya Tsh laki tano hadi sita (500,000 -600,000)
kutegemeana na ukubwa wa mfuniko, lakini hawa wakishaiba huwa wanaenda kuuza sh 500 kwa kilo hivyo
unakuta gharama kubwa inabaki kwetu sisi tunaotoa huduma hii” alisema Lyaro

“mifuniko ya chemba za Majitaka ni muhimu kwa uhifadhi wa Majitaka na pia kuzuia uchafu huo kutapakaa
ovyo mitaani, hivyo kuendelea kushamiri kwa biashara hiyo kunatupa wasiwasi wa uwezekano wa
magonjwa ya mlipuko utakaosababishwa na utiririshwaji wa Majitaka ovyo mitaani” alifafanua Lyaro
Aliongeza kwa kusema mapambano ya uhujumu katika miundombinu ya DAWASCO bado ni kubwa na
inahitaji ushirikiano wa pamoja kati ya wananchi, viongozi husika pamoja na DAWASCO katika kulinda na
kuhifadhi miundombinu ya Majisafi na Majitaka.
Katika tukio hilo Meneja Mkuu wa kiwanda hicho Raju N. Chita na Meneja utumishi Idrisa Ally
wamekamatwa na kufikishwa kituo cha polisi kijitonyama na kufunguliwa Jalada namba KJN/1786/2015
kwa hatua zaidi kisheria.
safi sanaaa...Nimefurahi sana...Japo nilikuwa naamini kuwa tu hili suala Viongozi wanalifungia macho sababu walikuwa wanajua wazi wapi hii mifuniko ya maji taka inapelekwa...
ReplyDeleteMabarabarani Mifuniko hii inapotolewa imekuwa ikisababisha hata ajali wakati mwingine kutokana na mashimo yake kuwa wazi na kutojua usiku.
Ningeomba Walipishwe mabilioni yatakayotosheleza kurudisha mifuniko yote ya majitaka iliyoibiwa Dar nzima...Shame on them