Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapnduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kufungua maonesho ya maadhimisho ya kutimia miaka 90 ya Skuli ya sekondari ya Benbella leo Skulini hapo(kushoto) ni Dk.Yussuf Nuhu Pandu Mwenyekiti wa Maonesho na (kulia) Rais wa Wanafunzi wa Skuli ya Benbella Awatif Duchi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapnduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiangalia maonesho ya maadhimisho ya kutimia miaka 90 ya Skuli ya sekondari ya Benbella leo Skulini hapo(kushoto) ni Dk.Yussuf Nuhu Pandu Mwenyekiti wa Maonesho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ki ukweli, Zanzibar ni mji mzuri sana na unaokua kwa kasi kubwa sana. Nafikiri unakua sana kuzidi Bara. Halafu hata masuala ya ufisadi ufisadi yameshamiri sana Bara kuliko zanzibar. Najiuliza sijui ni kwa nini

    ReplyDelete
  2. Mdau hapo juu sikubaliani na maelezo yako. Nadhani kama kukuwa kwa mji wa Zanzibar ni taratibu sana siyo kwa kasi ya hivyo ulivyoeleza, pia sasa hivi masuala ya ufisadi ufisadi ndio yanazidi kushika hatamu, maana Zanzibar ya miaka hiyo from 1980's backwards sio hii tuliyonayo leo, hii naweza kusema imetokana na ujio wa wahamiaji wengi kutoka bara, ambapo kwa kiasi fulani kumeathiri mila na desturi halisi za utamaduni na maadili mazima ya kizanzibari, vitendo vya wizi, uhuni, dhuluma n.k. havikuwepo miaka hiyo, uaminifu ndio miongoni mwa sifa kuu za Zanzibar miaka hiyo, leo hii mtu unaishi roho mkononi uwe njiani au hata kwako. Sasa sijuwi wewe ratio yako umeicalculate vipi au katika asilimia ngapi, maana Bara ni kubwa zaidi kuliko Zanzibar. Na kama umefanya research sijuwi ni kwa miaka ipi au kwa muda gani. Lakini ile Zanzibar tulokuwa tukijivunia ni njema atakae na aje, sio hii ya leo ambayo haina tofauti na ule usemi wa ndani ya mabasi ya Bara ya enzi hizo...abiria chunga mzigo wako.

    ReplyDelete
  3. Jamani ankal
    MIAKA 90 wakati hivi majuzi tu ndio kwanza tumesherehekea miaka 53 ya uhuru!Ina maana hi shule hata akina Sultani waliikuta achilia mbali mkoloni! Jamani tuwe makini!

    ReplyDelete
  4. Mdau wa tatu hapo juu usianze kulinganisha miaka 53 ya Uhuru na hiyo 90 ya Skuli ya Ben Bella. Kumbuka Skuli hiyo ilikuwepo na ingalipo tangu enzi hizo kabla ya Uhuru au hata Mapinduzi ya Zanzibar, si hiyo tu kuna Skuli kadhaa mathalan Forodhani, Haile Salasie, Tumekuja na nyingi nyinginezo khasa zilizopo katika mji mkongwe (Stone Town), baadhi zimekuwepo kwa miaka mingi sana na pengine kuizidi hiyo 53 ya Uhuru uliyoifanyia comparison. Hivyo usishangae kuona hiyo imetimiza miaka 90. Sultani si alihamia tu arround 1840's na kukuta majengo mengi yakiwa tayari yapo zikiwemo Skuli hizo n.k.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...