WADAU wa sanaa ndani na nje ya mkoa
wa Mbeya wameombwa kutoa ushirikiano kwa wasanii wa filamu mkoani hapa kwa
kununua kazi zinazofanywa na kuacha kasumba kuwa filamu bora zinaweza
kutengenezwa na wasanii walioko Dra es salaam pekee.
Mwongozaji wa filamu wa kampuni ya
Pritauj Filim Prince Hekela alitoa rai hiyo jana alipokuwa akitambulisha Filamu
mpya ya Vanilla iliyochezwa na wasanii kutoka mkoani Mbeya.
Prince Hekela alisema kumekuwa na
kasumba ya baadhi ya wadau kuamini filamu nzuri ni zile zinazochezwa na wasanii
wa Dar es salaam jambo alilosema limekuwa likididimiza sana wasanii wa mikoani.
Alisema ni wakati kwa wadau hao
kutambua kuwa ubora wa filamu hautokanani na mahali anakofanyia kazi zake
msanii,bali umakini na maandalizo bora ndiyo msingi wa kutengenezwa kwa filamu
bora.
Akizungumzia filamu ya Vanila
aliyosema tayari imeingizwa sokoni,alisema imeandaliwa katika mazingira yenye
kuzingatia staha hivyo haina vipande vyenye kuonesha aibu kiasi cha familia
kushindwa kuitazama kwa pamoja.
“Vanilla ni filamu ambayo hata
ukienda kuonesha uwanjani hakuna kinachozuia.Kwa nyumbani hata awepo baba mama
na watoto wanaweza kuiangalia kwa pamoja.Na ina mafundisho ya kila mtu
kulinagana na umri wake”
“Muhimu pia wadau watambue kuwa
tumejipanga kuhakikisha tunaleta burudani nzuri kutokana na filamu zetu.Ndiyo
sababu hata katika Vanila utaona tumechanganya wasanii wapya na wa
zamani.Wasanii wapya ambao wamefanya vizuri sana katika filamu hii ni pamoja na
Issa Ngoda,Regina Mwinyi, Kelvin Kaziyandege na Joachim Nyambo.Lakini pia
tumemshirikisha mwanadada Riyama Ally ambaye ni mkongwe katika sanaa”
alisisitiza Hekela.
Kwa upande wake mmoja wa wasanii
waliocheza filamu ya Vanila Joachim Nyambo alisisitiza kuwa filamu hiyo imekuja
kuwadhihirishia wadau kuwa kazi nzuri ya sanaa inaweza pia kufanyika mikoani.
Nyambo aliwasihi wadau kuendelea
kushirikiana na wasanii mikoani wanaoonekana kukuza sanaa kwa kuwa michango ya
hali na mali ili kuwezesha kukua kwa sanaa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...