Katibu Mkuu wa Divisheni ya Afrika Mashariki na kati wa Kanisa la Waadiventista Wasabato, Dkt. Nathaniel Walemba, akifungua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la kanisa la Waadiventista Wasabato Kigamboni jana mchana, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya extra vaganza yanayoendelea katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Divisheni ya
Afrika Mashariki na kati wa Kanisa la Waadiventista Wasabato, Dkt. Nathaniel
Walemba, (wa nne kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi
mbalimbali wa Kanisa la Wasabato kigamboni, wazee wa kanisa hilo na baadhi ya
washiriki wa kanisa hilo, jana mchana mara baada ya kuweka jiwe la msingi. Wa
nne kutoka kulia ni Katibu wa Union ya Kusini Mwa Tanzania, Mchungaji James Machage.
Vijana wa Chama cha Watafuta Njia(PF), kutoka kanisa la Waadiventista Wasabato Kigamboni, wakimvalisha Skafu Mwenyekti wa Konference ya Kusini Mwa Tanzania, Mchungaji Mark Marekana (wa pili kutoka kulia), kabla ya kuweka jiwe la msingi katika kanisa la waadventista wasabato Kigamboni,jana mchana.
Picha na Lisso Ibrahim Biseko
Katibu Mkuu wa Unioni ya Kaskazini mwa Tanzania, Mchungaji Davis Fue, akiangalia ramani ya jengo la kanisa la Waadventista Wasabato litakavyokuwa mara baada ya kumalizika, wakati wa uwekaji jiwe la msingi la kanisa hilo jana mchana, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Extra Vaganza, ambayo yanafanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwaya ya Kanisa la Waadventista Wasabato Kigamboni, wakiimba kabla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Kanisa la Waadventista Wasabato Kigamboni. Jiwe hilo la msingi liliwekwa jana na Katibu Mkuu wa Divisheni ya Afrika Mashariki na kati wa Kanisa la Waadiventista Wasabato, Dkt. Nathaniel Walemba kwa niaba ya Mwenyekiti wa Divisheni ya Afrika Mashariki na kati wa Kanisa la Waadiventista Wasabato, Mchungaji, Dkt. Blasious Ruguri.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...