Bendi ya muziki INAFRIKA BAND aka "Wazee wa Indege" kutoka jiji Dar es salaam, imelitingisha jiji la Bremen, nchini Ujerumani katika onyesho liliofanyika usiku wa 13 Februari 2015 katika ukumbi mkubwa wa Musik-Theater mjini humo.
Bendi hiyo kutoka Chang'ombe ilisimama jukwaani na kuziteka nyoyo za maelfu ya wapenzi wa muziki kiasi cha kutajwa kuwa bendi
bora ya muziki wa Folk na radio Funkhaus-Europe kutokana na vionjo vya mitindo ya muziki wa asili wa makabila ya Kitanzania vilivyotumiwa na Inafrika Band katika kuteka yonyo za washabiki kila kuona duniani.
Inafrika Band, ambayo imefanikiwa kuliweka jina la Tanzania katika tufe la dunia kwa kutumia mitindo yake ya vionjo vya kiasilia, inaongoza katika kufanya tour ndefu duniani,
Hadi sasa wameshafanya ziara katika mabara yote duniani kuanzia Afrika, Austalia, Amerika, Asia Ulaya na visiwa vya Karebiki.
Wakali hawa wa mdundo inayokubalika kimataifa wanatisha na kuzoa washabiki kwa dhoruba kali la mtindo wao wa muziki.
Inafrika band inatuwakilisha na hivi sasa bado wapo katika ziara ndefu ughaibuni kuhakikisha kuwa muzikiwa wao unasikika kila kona nje ya mipaka ya Tanzania.
Usikose kuwasikiliza Inafrika Band "Wazee wa Indege" kupitia http://www.inafrikaband.co.tz
Pia unaweza kuwapa hi kupitia info@inafrikaband.co.tz ii
INAFRIKA BAND aka "Wazee wa Indege" kutoka jiji Dar es salaam wakifanya onesho kubwa katika jiji la Bremen, nchini Ujerumani, usiku wa 13 Februari 2015 katika ukumbi mkubwa wa Musik-Theater jijini humo.
Ngoma ya "Indege" ikivurumishwa
Kazi mbele kwa mbele
Nyomi ya mashabiki wa jiji la Bremen
Wakubwa Inafrika Band basi tupieni pia video clips zenu YouTube kwa kufungua account.
ReplyDeleteMaana vitu mnavyofanya ni vya uhakika sana.
Mdau
Muziki wa Kweli