Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii
‘Usilolijua ni sawa na usiku wa giza’ msemo huu una maana kwani kitu usichokijua huwezi ukajadili kutokana na kutokielewa.
Katika pitapita mitaani hasa katika maeneo ya masoko katika jiji la Dar es Salaam kuna mtu aliyejitambulisha kwa jina la Julius Methew alienileza kuwa hakuna sehemu yeyote katika nchi za Afrika ambayo takataka zake zinatoka mashambani na kupelekwa mijini isipokuwa Tanzania ambayo ameitaja kuwa ni nchi ya kwanza kwa Afrika inayopokea takataka za mashambani kuingiza mijini.
Mathew anasema taka nyingi zinazozalishwa vijijini zinakuja katika jiji la Dar es Salaam ambapo kila sehemu ya masoko utakuta uchafu na mwingine kuingia katika mitaa mbalimbali kutokana na kuchukua huduma katika masoko hayo.
Anasema kuwa na uchafu katika jiji la Dar es Salaam ni kutokana na kutokuwa na mfumo wa kutunza mazingira na mwisho wa siku watu wanailaumu serikali kwa kushindwa kukusanya taka katika mitaa.
Aidha anasema vijiji ambavyo vinazalisha bidhaa mbalimbali vina kuwa na usafi kutokana na takataka zao kuleta mijini.
Julius anasema kuwa ndizi mbivu zinapoletwa katika jiji la Dar es Salaam zinakuja zikiwa zimefunikwa na majani ya mgomba lakini mwisho wa siku majani yanabaki sokoni,hapo ndipo utakuta ni tatizo la kuwa na taka nyingi katika jiji letu.
“Mfumo huu wa kuchukua taka vijijini utafanya jiji kuendelea kuwa na uchafu miaka yote na hakuna suluhu itakayowezesha kuondokana”anasema Methew.
Mathew anasema nyanya nazo zinazalishwa zinakuja katika tenga zikiwa zina majani lakini mwisho wa siku nyanya zinaondoka majani yanabaki sokoni hili ni tatizo katika jiji la kuweza kuondokana na uchafu wa masoko na mitaani.
Aidha anaeleza kuwa teknolojia imezidi kukua lakini bado watu wanatumia tenga ,majani ya migomba ,majani ya mpunga kusafirishia bidhaa na mwisho wa siku bidhaa zinaisha lakini mwisho wake ni kupata majani.tenga na majani ya mpunga katika mitaa.
Anasema suluhu yake ni serikali kupiga marufu uingizaji wa bidhaa ambazo zinakuwa na takataka kwa kutumia mfumo wa kuweka katika boksi ambapo boksi inaweza ikaondolewa bidhaa na boksi kuendelea kuwa bidhaa na kuzalisha bidhaa nyingine.
Uchafu unatisha, uchafu mwingi tunaoona tikiamua tunaweza kuondokana nao.
ReplyDeleteExellent
ReplyDelete