Wananchi wakiangalia jengo la ofisi ndogo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) la Lumumba, ambapo kilizaliwa chama cha Tanu lililobomolewa kupisha ujenzi wa jengo jipya la chama hicho Dar es Salaam jana
Dotto Mwaibale
JENGO la ofisi ndogo la Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mtaa wa Lumumba Dar es Salaam ambako ndiko kilizaliwa Chama cha Tanu limebomolewa ili kupisha ujenzi wa jengo jipya la chama hicho.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye alisema jengo hilo limebomolewa kwa ajili ya matengenezo ya kawaida.
"Tunachokifanya katika jengo hili ni ukarabati wa kawaida,"alisema Nape wakati akielezea jengo hilo ambalo limebomolewa jana kwa kutumia tingatinga.
Kutokana na kubolewa kwa jengo hilo , viongozi wa ngazi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrhaman Kinana , watakuwa katika Jengo la Umoja wa Vijana wa chama lililopo barabara ya Morogoro, wakati ukarabati wa jengo hilo lililobomolewa ukiendelea.
Awali baadhi ya makada wa chama hicho waliokuwa eneo hilo, walidai kuwa jengo hilo la Tanu limebolewa ili kupisha ujenzi wa jengo la kisasa ambalo litatumika kwa ajili ya kitega uchumi.
Makada hao walisema jengo hilo litakapokamilika litakuwa la kisasa zaidi tofauti na jengo ambalo lilikuwepo eneo hilo.
Kwa hili wana CCM wenzangu mmeharibu. Hii ilitakiwa iachwe kama kumbukumbu ya vizazi vijavyo. Fedha tunayo yakutosha ni vyema tungenunua eneo na kujenga lakini hapo tungepaacha palivyo. Mmeboronga hapa
ReplyDeleteKwani "ukarabati" tafsiri yake kwa Kiswahili ni nini? sasa inakuwaje jingo lina vunjwa lote na kujengwa jipya jingine halafu bado bwana nape ana kaririwa akisema huo ni ukarabati,mimi nilififkiri ukarabati ni "renovation" kwa lugha ya watu kumbe ni"demolition" jamani nisaidieni wenye kujua lugha hizi mbili mwenzenu nilikuwa nasinzia darasani sasa najuta na kupata shida kweli kweli.
ReplyDeletemdau.
machinga,kariakoo
Tragic! Nakubaliana na Anonymous aliondika hapo juu, wangeaacha hilo jengo kama historia ya ukumbusho, nk.
ReplyDeleteThis is such a great loss, and the decision makers have no inkling for the value of history or living legends.
Arrogance to say the least. May the founding fathers of TANU and the late John Rupia who gave that house to TANU and after that CCM, rest in peace. Nape should at least make sure to dedicate a room in the new building that explains the history of the party that honours the founding fathers and mothers such as Bibi Titi Mohammed.