Mwigizaji Julianne Moore ndiye mshindi wa mwaka huu wa waigizaji sinema wa kike na kushinda tuzo ya Oscar kwa kucheza vyema kwenye filamu ya "Still Alice."
Usiku wa kuamka leo huko Marekani, Moore amewashinda Felicity Jones ("The Theory of Everyting"), Marion Cotillard ("Two Days, One Night"), Reese Witherspoon ("Wild") na Rosamund Pike ("Gone Girl) katika kinyang'anyiro hicho. Awali alipendekezwa mara tano kugombea tuzo hiyo ya juu katika tasnia ya sinema duniani, na ni mmoja wa waigizaji 11 ambao wamewahi kupendekezwa kushindania tuzo hiyo mara mbili katika mwaka mmoja wa 2003, kwa umahiri wake katika filamu za "Far From Heaven" na "The Hours". Hii ni mara ya kwanza kwa Moore kushinda tuzo hiyo.
Huyu Dada Julianne Moore namkubali sana, kwa wale wanao penda comedy, family movie anaweza sana. Inakipaji cha hali ya juu. sinema zake utazani za kweli.
ReplyDelete