Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Halima Ramadhan Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo Tegeta jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, ikiwa ni moja ya misaada inayotolewa katika vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima wakati wa msimu huu wa maadalizi ya Tamasha la Pasaka linalotimiza miaka 15 tangu lianzishwe.

Msama amekabidhi misaada hiyo kwa vituo vitano vya kulelea watoto waishio katika mazingira magumu,makabidhiano ya misaada hiyo ilifanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo,Kinondoni jijini Dar.

Msama alisema kuw maandalizi ya tamasha hili yanaendelea vyema mpaka sasa,na kwamba tamasha hilo linatarajiwa kufanyika jijini Dar April 7 2105,ambapo litashirikisha waimbaji mbalimbali wa Kimataifa na wa Nchini,aliongeza kuwa ili kunogesha zaidi tamasha hilo pia kutakuwepo na michezo mbalimbali itakayochezwa ikiwemo na kukabidhi zawadi na vikombe kwa washiriki wa tamasha hilo.

katika hatua nyingine Bwa.Alex Msama amelaani matukio ya mauaji ya Albino hapa nchini,ameiomba Serikali kutilia mkazo katika janga hilo ambalo limekuwa likiibua na kuzua gumzo miongoni mwa jamii,hivyo ameiomba Serikali kuwashughulikia ipasavyo wahusika wote waliofanya na wanaofanya ukatili huo ambao ni kinyume kabisa na maadili ya nchi yetu,na ikibidi kukomesha kabisa matukio hayo ambayo yamekuwa yakilitia aibu Taifa letu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...