BABA mzazi wa msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Dully Sykes, mzee Ebby Sykes amefariki dunia jioni ya leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Presha.
Ebby Sykes alikuwa muimbaji na mpiga gitaa mashuhuri na ndiye anayedaiwa kumfundisha mambo mengi ya muziki mwanae Dully Sykes.
Sykes alizaliwa February 24, 1952 ambapo tarehe hiyo mwaka huu alikuwa anatimiza miaka 63.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
-Amen
Inna Lillahi Wainna Ilay Rajiuun. Mwenyeez Mungu amjaaliye safari ya kheri, amughufiri kwa yote, amnusuru adhabudhe na amjaaliye palipo pema peponi - Ameen. Pole sana Dully, poleni wanafamilia wote na kila aliyekhusu ama kuguswa na msiba huu. Daima tukumbuke, duniani ni mapito na akhera marejeo na ndio khatamia yetu.
ReplyDelete