Taarifa iliyotufikia mapema leo,inaeleza kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la ‘Chamber Squad’, Moses Bushagama ‘Mez B’, amefariki dunia leo asubuhi huko Mkoani Dodoma baada ya kusumbuliwa na Homa ya mapafu kwa muda mrefu. Taarifa ya kifo cha Mez B zimethibitishwa na mama yake mzazi, na kwamba alikuwa amelazwa kwenye Hospitali ya Mwananchi.

Mez B amewahi kulazwa na kuruhusiwa mara kadhaa katika hospitali ya Dodoma na hivi karibuni alizidiwa na kulazwa mkoani humo mpaka umauti ulivyompata.

Baadhi ya nyimbo alizowahi kuimba Mez B ni pamoja na ‘Fikiria’, ‘Kama Vipi’, ‘Kikuku’, ‘Shemeji’ ‘Nimekubali’ pamoja na ‘Ghetto langu’ aliyoshirikishwa na Marehemu Albert Mangwea.

Huyu ni msanii wa pili kufariki kutoka kundi la chamber squad. Miaka miwili iliyopita kundi hilo liliomboleza kifo cha mwenzao Albert Mangwea ‘Ngwea’ huku Mez B akiwa mstari wa mbele wakati wa mazishi yake.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...