MWIMBAJI mahiri wa nyimbo za Injili nchini, Upendo Kilahiro
amesema kuwa endapo atapata nafasi ya kushiriki kwenye miaka 15 ya Tamasha la Pasaka
mwaka huu, ataimba nyimbo zilizopo katika albamu yake mpya inayotarajia
kukamilika hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Kilahiro tamasha hilo ni maalum kwa sababu linatimiza miaka 15
tangu kuanzishwa kwake hivyo akipata nafasi katika tamasha hilo ataimba nyimbo mpya kama zawadi kwa watanzania.
Alipotakiwa kuitaja albamu hiyo na baadhi ya
nyimbo zilizomo humo alisema ni mapema kuitaja hata hivyo nia yake ni
kuwashitukiza watanzania watakaopata fursa ya kushiriki tamasha hilo ambalo
litakuwa la aina yake.
Alisema iwapo atapata nafasi katika tamasha
la mwaka huu ataimba nyimbo hizo mpya na zile za zamani ambazo zinatamba katika
ulimwengu wa muziki wa injili huku akiwaomba watanzania kufika kwa wingi katika
tamasha hilo litakuwa tofauti na mengine yaliyowahi kufanyika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...