Na Victor Mariki – Ofisi ya Makamu wa Rais
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, limetoa amri ya kfungwa shughuli
za uzalishaji katika Kiwanda cha nguo cha 21st Century Limited kilichopo Kihonda Mkoani
Morogoro leo ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira.
Hatua hiyo imechukuliwa kufuatiwa na kupuuzwa kwa maelekezo na maagizo ya
mazingira yaliyokuwa yakitolewa nyakati tofautit tofauti na Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa Morogoro na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Morogo .
Kiwanda hicho chenye wafanyakazi 1779 kiliagizwa na kuelekezwa tangu mwaka 2006
mamlaka hizo kutumia mitambo ya kutibu majitaka yake kabla ya kuyatiririsha kwenye Mto
Ngerengere ili kuhepusha jamii inayotumia vyanzo vya maji hayo na madhara ya kiafya.
Aidha Taarifa ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ilifafanuwa kuwa
mitambo ya kutibu sumu ya majitaka kiwandani hapo haina uwezo wa kutosha kutibu sumu
zinazozalishwa na shughuli za uendeshaji wa kiwanda hicho.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa kufungwa kwa kiwanda hicho ni sehemu ya Utekelezaji wa
Sheria ya Mazingira Na. 20 ya mwaka 2004 pamoja na Kanuni za Mazingira ya mwaka 2007
ambazo zinavitaka viwanda kutibu majitaka yake hadi kufikia viwango vilivyowekwa kabla ya
kumwaga au kutiririsha maji hayo kwenye mazingira.
Hawa jamaa wengine wanajiona kama vile wapo juu ya sheria.
ReplyDeleteKiwanda kinachafua mazingira, wameambiwa kutekeleza amri lakini bado wanafanya dharau.
Wanatuumiza sisi wananchi.
Tunapongeza kwa sheria kuchukua mkondo wake, labda na wengine watafuata.
Lo afadhali serikali imeto makucha katika hili. Huku nchi za magharibi wasingejaribu hata tone lakini kwa madharau yao Bongo wanataka kuangamiza watu na mali asilia kwa cancer na magojwa ya ajabu ya ngozi- kama ilivyotokea kule Mkoani Mara.
ReplyDeleteAhsante sana Serikali kwa fundisho hili. Kazeni uzi uleule.
Hongera..serikali hapo naona imefanya linalotakiwa..nadhania wakati umefika sasa kuangalia hata watu wanaotupa taka ovyo kwenye mito.
ReplyDeletembona bado kinafnya kazi jamani
ReplyDelete