Na Victor Mariki – Ofisi ya Makamu wa Rais

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, limetoa amri ya kfungwa shughuli za uzalishaji katika Kiwanda cha nguo cha 21st Century Limited kilichopo Kihonda Mkoani Morogoro leo ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira.

Hatua hiyo imechukuliwa kufuatiwa na kupuuzwa kwa maelekezo na maagizo ya mazingira yaliyokuwa yakitolewa nyakati tofautit tofauti na Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Morogo .

Kiwanda hicho chenye wafanyakazi 1779 kiliagizwa na kuelekezwa tangu mwaka 2006 mamlaka hizo kutumia mitambo ya kutibu majitaka yake kabla ya kuyatiririsha kwenye Mto Ngerengere ili kuhepusha jamii inayotumia vyanzo vya maji hayo na madhara ya kiafya.

Aidha Taarifa ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ilifafanuwa kuwa mitambo ya kutibu sumu ya majitaka kiwandani hapo haina uwezo wa kutosha kutibu sumu zinazozalishwa na shughuli za uendeshaji wa kiwanda hicho.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa kufungwa kwa kiwanda hicho ni sehemu ya Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira Na. 20 ya mwaka 2004 pamoja na Kanuni za Mazingira ya mwaka 2007 ambazo zinavitaka viwanda kutibu majitaka yake hadi kufikia viwango vilivyowekwa kabla ya kumwaga au kutiririsha maji hayo kwenye mazingira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hawa jamaa wengine wanajiona kama vile wapo juu ya sheria.

    Kiwanda kinachafua mazingira, wameambiwa kutekeleza amri lakini bado wanafanya dharau.

    Wanatuumiza sisi wananchi.

    Tunapongeza kwa sheria kuchukua mkondo wake, labda na wengine watafuata.

    ReplyDelete
  2. Lo afadhali serikali imeto makucha katika hili. Huku nchi za magharibi wasingejaribu hata tone lakini kwa madharau yao Bongo wanataka kuangamiza watu na mali asilia kwa cancer na magojwa ya ajabu ya ngozi- kama ilivyotokea kule Mkoani Mara.
    Ahsante sana Serikali kwa fundisho hili. Kazeni uzi uleule.

    ReplyDelete
  3. Hongera..serikali hapo naona imefanya linalotakiwa..nadhania wakati umefika sasa kuangalia hata watu wanaotupa taka ovyo kwenye mito.

    ReplyDelete
  4. mbona bado kinafnya kazi jamani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...