Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitika kutangaza kusitishwa kwa muda huduma ya treni ya Jiji  kuanzia leo  Jumatano jioni Februari 25 hadi  Jumatatu  Machi 02, 2015 itakapoanza tena.

Kwa mujibu  wa taarifa ya Uongozi wa TRL iliotolewa jioni  leo Februari 25,  2015 uamuzi wa kusitisha huduma hiyo umesababishwa  na vichwa  viwili vya treni hiyo kuharibika na kuhitaji matengenezo makubwa katika Karakana Kuu ya Morogoro .
Taarifa imefafanua kuwa kwa vile kimebaki  kichwa kimoja huduma hiyo haiwezi kuendelea hadi vichwa hivyo viwili vitakapo maliza kukarabatiwa siku ya Jumamosi huko Morogoro.
Kwa kawaida treni ya Jiji hutumia vichwa  viwili wakati inapotoa huduma kati ya stesheni za Ubungo Maziwa na Stesheni kuu ya Dar, wakati kile  cha tatu huwa cha akiba endapo dharura itakipata kichwa kimoja wapo  wakati huduma inaendelea.
Aidha Uongozi wa TRL unawaomba  radhi wateja wake na wananchi  kwa jumla hasa wa eneo la Jiji waliokuwa wamezoeya kupata huduma hiyo kila siku kwa  usumbufu  utakajiotekeza .
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji ,
Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu
Dar es Salaam,
Februari  25, 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...