Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mchana wa leo, Jumatano, Februari 25, 2015, ametembelea na kuweka mashahada ya maua ya marais wa tatu wa Zambia katika eneo la Mazishi ya Marais katikati ya Jiji la Lusaka, Zambia.
Rais Kikwete ametembelea na kuweka mashada ya maua katika makaburi ya Marais Frederick Chiluba, Levy Mwanawasa na Michael Sata ikiwa ni tendo lake la kwanza mara baada ya kuwasili nchini Zambia kuanza ziara rasmi ya siku mbili nchini humo kwa mwaliko wa Rais Edgar Lungu.
Rais Kikwete ameanza kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais Sata, likifuatia kaburi la Rais Mwanawasa ambako pia ameweka saini kwenye kitabu cha rambirambi na hatimaye kwenye kaburi la Rais Chiluba.
Mapema Rais Kikwete amewasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda kiasi cha saa sita mchana (kwa saa za Zambia) na kupolekewa kwa shangwe pamoja na mvua kubwa iliyokuwa inanyesha uwanjani hapo.
Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja huo, Rais Kikwete ambaye anaandamana na mkewe Mama Salma Kikwete, amepokelewa na mwenyeji wake, Rais Lungu, akapigiwa mizinga 21 ya heshima na kukagua gwaride la Jeshi la Ulinzi la Zambia.
Baadaye, Rais Kikwete amefanya mazungumzo rasmi ya Kiserikali na Rais Lungu na kuhudhuria Dhifa ya Kitaifa kwenye Ikulu ya nchi hiyo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Rais wa Zambia Michael Sata aliyefariki mwaka jana katika eneo la maziko ya viongozi wa kitaifa jijini Lusaka Zambia leo.Rais Kikwete alitumia wasaa huo pia kuweka shada la maua katika marais wa Zambia waliofariki Marehemu Frederick Chiluba na Levy Mwanawasa. Picha na Freddy Maro
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...