Msama ameongeza kuwa hivi sasa wako katika mazungumzo na waimbaji wa muziki wa injili kutoka nje ya nchi hasa kule Afrika Kusini na Uingereza, waimbaji ambao wako katika mazungumza na kampuni ya Msama Promotion ni Solomon Mahlangu, Rebecca Malope, Keke Pofolo na wengine wote kutoka nchini Afrika Kusini.

Msama alisema kuwa idadi ya mikoa ambayo imeomba iandae onesho la miaka 15 ya Tamasha la Pasaka sasa imefikia 17,amesema Tamasha la Pasaka kwa mwaka huu litakuwa la aina yake tangu walipoanzisha tamasha lao mwaka 2000.
 
“Tumepokea maombi ya wadau kutoka mikoa 17 wakitaka tupeleke Tamasha la Pasaka mikoani kwao. Tunachofanya kwenye kamati yangu ni kupokea maoni kwa njia mbalimbali kwa wadau wetu wa huko.
 
 “Lakini si kupendekezwa au kuombwa tu na wadau ndiyo kigezo cha kupewa nafasi, lazima tuangalie na mazingira ya mkoa husika katika mambo ya matamasha,” alisema Msama.Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Morogoro, Rukwa,  Mara, Singida, Arusha, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Tanga, Dar s Salaam, Mtwara, Mwanza, Dodoma, Tabora, Shinyanga, Kilimanjaro na Zanzibar.

  Alisema kamati yake inatarajia kukutana Jumatano wiki hii na kufanya tathmini ya maombi kwa wadau wao wa maeneo hayo ili kupata mikoa sahihi ambayo tamasha hilo litafanyika mwaka huu.
 
Tamasha la Pasaka linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la Krismas kila mwaka, lakini wanataka Tamasha la Pasaka mwaka huu liwe bora zaidi kwa sababu wanasherehekea miaka 15 tangu waanzishe tamasha hilo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...