Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Kinondoni ,Grace
Temba akizungumza leo na wajasirimali wa Mkoa wa Kinondoni (hawapo pichani) juu ya faida ya kujiunga
na mfuko huo kupitia Mtandao wa ASEE iliyofanyika katika ukumbi Pricess ,Sinza
Jijini Dar es Salaam.
Afisa Matekelezo na Uratibu wa NHIF,Catherine Masingisa
akitoa maada kwa wajasirimali wa Mkoa wa Kinondoni (hawapo pichani) namna ya kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya kupitia vikundi vya ujasiriamali iliyofanyika
Katika Ukumbi wa Princes ,Sinza jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wajasiriamli wakisikiliza maada
kutoka kwa maafisa wa NHIF katika ukumbi wa Princess ,Sinza jijini Dar es
Salaam.Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.
======= ======== ====== =========
Na Chalila Kibuda.
Mfuko wa
taifa wa Bima ya Afya (NHIF)umewataka wajasiriamali wajiunge katika Mtandao wa
Jamii wa Huduma ya Afya (ASEE)ili waweze kupata huduma ya afya kwa kuchangia
Sh.78,600 kwa mwaka mzima.
Akizungumza
na wajasiriamali wa Mkoa wa Kinondoni,Afisa Matekelezo na Uratibu ,Catherine
Masingisa amesema si wakati wote mjasiriamali hawezi akawa fedha ya matibabu
kujiunga na mfuko kunamfanya aweze kupata matibu katika vituo vyote
vilivyosajiliwa na mfuko huo.
Masingisa
amesema mpango huo wa kurasimisha wajasirimali kupitia mtandao unatambulika
kama Kikoa kutokana na michango yao inakusanywa sehemu moja na kupelekwa katika
mfuko wa NHIF.
Amesema
watanzania wote wanatakiwa kuwa kadi ya mfuko wa bima ya afya ili kumuwezesha
kila mtu kupata matibabu sehemu yeyote kutokana na hali ya uchumi,kwa sababu mtu
hawezi kuwa na fedha wakati wote.
Kwa upande
wa Afisa Mtekelezo na Uratibu,Tumaini Geofray amesema mfuko umejipanga kufikia
wananchi wote juu ya kuwaelimisha faida ya kujiiunga na mfuko huo kupitia vikundi ili kupata urahisi wa kuratibu
zoezi hilo


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...