Na Bashir Yakub
Kuomba talaka si dhambi. Kama lingekuwa dhambi sheria isingeruhusu jambo hilo kwakuwa si kawaida ya sheria kuhamasisha madhambi. Ni kwasababu hii nasema kuwa atakayeona amebanwa basi aombe talaka. Si kosa hata kidogo kufanya hivyo isipokuwa ndivyo tunavyoelekezwa na sheria zetu tunazozipenda na kuziheshimu sana.
1. KUVUNJIKA KWA NDOA.
Kuvunjika kwa ndoa kwa mujibu wa sheria zetu za Tanzania kuna mazingira mengi. Baadhi ya mazingira hayo ni yale yaliyoorodheshwa kifungu cha 12 (a-e) cha Sheria ya ndoa ambayo ni pamoja na kifo cha mmoja wa wanandoa, talaka ambayo tunaiongelea lakini pia yapo mazingira mengine mengi.
2. AINA ZA TALAKA
Talaka twaweza kuzigawa katika makundi mawili nayo ni, talaka itolewayo nje ya mahakama ambayo hutokana na ndoa zilizo katika mfumo wa kimila na nyingine ni talaka itolewayo mahakamani ambayo sisi hapa tutaiongelea.
3. UKITAKA TALAKA FUATA HATUA HIZI.
( a ) Hatua ya kwanza kabisa kwa anayehitaji kupata talaka ni kupeleka malalamiko yako kwenye kitengo maalum kijulikanacho kama Bodi ya usuluhishi wa ndoa ambayo imeanzishwa na Sheria ya ndoa kifungu cha 102(1).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...