Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud, amewasili Dubai kwa ziara ya kikazi.
Akiwa Dubai, Mhe. Aboud atafanya mazungumzo na Kamati ya Maandalizi ya Maonyesho ya Biashara ya Dunia 2020 (World Expo2020).
Aidha, atafanya mazungumzo na Nd. Islam Balhabou, Mfanyabiashara Mtanzania ambaye amejitolea kufungua ofisi ya biashara ya Zanzibar (Trade Mission).
Pichani kulia ni Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai, akimkaribisha Mhe. Aboud, Dubai, na kushoto ni Nd. Islam Balhabou
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...