Na Bashir Yakub
Yapo
mambo ambayo huwaumiza watu vIchwa
yumkini yakiwa ni mambo madogo na ya kawaida. Tatizo mara nyingi huwa ni taarifa. Taarifa zikimfikia
mtu ndipo huhisi jambo ambalo
alikuwa halijui kuwa ni jepesi.
Lakini
kabla ya taarifa mtu huendelea kufikiria jambo hilo kwa ugumu.
Katika kipindi kama hiki kuwa na kitu kama pasipoti si jambo la anasa
au ufahari tena isipokuwa ni jambo
ambalo limeishaingia katika matumizi ya kawaida ya
kila siku ya walio wengi.
Hii ni kutokana na kukua kwa biashara za kimataifa, mawasiliano,
utalii,usafirishaji na kila kitu ambacho
husababisha watu kutoka nchi moja hadi
nyingine. Kwasasa kuwa na pasipoti hata kama huna safari ya hivi karibuni ni jambo
muhimu sana.
Yumkini usisubiri ikutokee
safari ya ghafla halafu ndio uanze kukimbizana
na pasipoti. Pasipoti inayo
manufaa mengi lakini moja ni kuwa
pasipoti ni mali kama mali nyingine.
Pasipoti inaweza kumdhamini mtu kama mali
nyingine inavyoweza kumdhamini mtu.Pasipoti ni amana tena amana ya kuaminika. Ni kutokana na umhimu huu nikaona leo nieleze pasipoti na namna ya kupata pasipoti. Kusoma Zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...