Na  Bashir  Yakub

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, zipo aina nyingi za ndoa. Pamoja na kuwa na aina nyingi za ndoa, ndoa hizi tunaweza kuzigawa katika makundi makuu mawili. Kwanza, ndoa za serikali(civil marriage) na Pili ni ndoa za kimila(customary marriage).

Ndoa za serikali ni zile ndoa zinazofungwa kwa mkuu wa Wilaya, Msajili wa ndoa pamoja na katika Ofisi nyingine za serikali kama Ubalozini n.k.

Ndoa za kimila ni zile ndoa zinazofungwa kulingana na taratibu za kabila la wahusika; kwa mfano ndoa za wahaya, wachaga, ndoa za wazaramo na ndoa nyingine zitokanazo na makabila mbalimbali. 

Ndoa za kidini pia zinaingia katika kundi hili la ndoa za kimila. Ndoa za kidini ni zile zinazofungwa kutokana  na imani ya dini za wahusika. Katika ndoa za dini kuna ndoa za kiislamu, kuna ndoa za kikiristo, ndoa za kibudha na dini nyingine nyingi wanazo ndoa zao. Mbali na aina hizo za ndoa nilizotaja hapo juu ipo aina nyingine ya ndoa ambayo kwa masikio ya wengi yaweza kuwa ngeni kwa wasomaji wetu  hapa.

Aina hii ya ndoa inapatikana katika kifungu cha 160 kifungu kidogo cha kwanza katika Sheria ya Ndoa. Kifungu hiki kinasema kuwa “Itakapothibitika kuwa mwanaume au mwanamke wameishi wote kwa miaka miwili au zaidi  katika hali ambayo maisha yao yamekuwa kama mume na mke, litajengwa wazo au dhana (presumption) kuwa watu hao wameoana.” 

Maana yake ni kuwa  mwanaume na mwanamke wakiishi wote kwa kipindi cha miaka miwili au zaidi bila kufunga ndoa, kwa mujibu wa sheria watu hao watahesabika kama watu waliooana  hata kama watu hao hawakufunga ndoa kanisani, msikitini au  serikalini.

Ni kwa ufupi sana tunaweza kusema kuwa wachumba au wapenzi wanaoishi kama mke na mume kwa kipindi cha miaka miwili au zaidi, hao wanahesabika kuwa wameoana na sheria inawalinda sawa kabisa na inavyomlinda mke na mume waliofunga ndoa ya kawaida.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Pika pakuwa

    ReplyDelete
  2. sio wanaume wa bongo hadi miaka 10 bado hawatakubali. Angalia nyumba nyingi hawajafunga ndoa na wameshakaa na wana watoto.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...