Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT),
ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba
(kushoto) akimsimika kwa kumkabidhi fimbo ya ulezi baada ya kumvalisha joho, kofia
na skafu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Nachingwea, mkoani Lindi, Mathias Chikawe, kuwa mlezi wa UWT katika wilaya yake
ya Nachingwea. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa UWT,
ilifanyika katika Ukumbi wa NR mjini Nachingwea leo. Wapili kulia ni Mkuu wa
wilaya hiyo, Regina Chonjo, na wapili kushoto ni mwanachama wa UWT wilayani
humo, ambaye pia ni Mke wa Waziri Chikawe, Profesa Amandina Lyamba
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo
(kushoto), Mke wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe, Profesa Amandina Lyamba (kulia)
wakilisakata rumba na wanachama wenzao wa Umoja wa Wanawake (UWT) wilayani humo
baada ya Mbunge wao kusimikwa rasmi na Mwenyekiti wa UWT Taifa, ambaye pia ni Waziri
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, kuwa mlezi wa UWT katika
wilaya yake ya Nachingwea. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa
UWT, ilifanyika katika Ukumbi wa NR mjini Nachingwea leo.
Mlezi wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya
Nachingwea, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa mwakilishi wa
UWT wilayani humo baada ya Waziri huyo kusimikwa na rasmi na Mwenyekiti UWT
Taifa, ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba
(kushoto kwa Chikawe), kuwa mlezi wa UWT wilayani humo. Sherehe hiyo
iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa UWT, ilifanyika katika Ukumbi wa NR
mjini Nachingwea leo
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT),
ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba
akizungumza kwa furaha wakati akitoa hotuba yake kwa wananchama wa UWT Wilaya
ya Nachingwea baada ya kumsimika Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia
ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) kuwa mlezi wa UWT
wilayani humo. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa UWT,
ilifanyika katika Ukumbi wa NR mjini Nachingwea leo. Katika hotuba yake hiyo,
Waziri Simba alimuomba Waziri Chikawe aendelee kuisaidia UWT wilayani humo kama
alivyokuwa anafanya awali. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT, Mkoa wa Lindi, Faudhia
Chiwangu.
Mlezi wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya
Nachingwea, ambaye pia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe
akiwashukuru wanachama wa UWT wilayani humo kwa kumchagua kuwa mlezi wa umoja
wao katika sherehe ya kusimikwa kwake iliyofanyika mjini Nachingwea leo. Katika
hotuba yake, Waziri Chikawe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, aliwaomba
wanachama hao kuwa na ushirikiano kwa kuijenga CCM, pamoja na kuhakikisha wanawahamasisha
wananchi jimboni humo kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili kujiandaa
kwa kuipigia kura Katiba iliyopendekezwa pamoja na Uchaguzi Mkuu ujao. Kulia ni
Mwenyekiti UWT Taifa, ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto, Sophia Simba ambaye alimsimika mlezi huyo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya
hiyo, Regina Chonjo
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba (kushoto) akimsimika kwa kumvalisha joho
la ulezi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la
Nachingwea, mkoani Lindi, Mathias Chikawe, kuwa mlezi wa UWT katika wilaya yake
ya Nachingwea. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa UWT,
ilifanyika katika Ukumbi wa NR mjini Nachingwea leo. Picha zote na Felix Mwagara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...