Na Bashir Yakub
Ndoa inapovunjika kuna kuna mambo makuu matatu ambayo hutokea
yakiwa kama matokeo ya ndoa hiyo kuvunjika. Kwanza ni kugawana
mali walizochuma wanandoa , pili hifadhi ya watoto na tatu matunzo
ya watoto. Haya ni matokeo ya kuvunjika kwa ndoa, mengine zaidi
kuhusu kuvunjika kwa ndoa tutayaona hapa wakati nikieleza
mgawanyo wa mali za wanandoa.
1.MALI ZIPI HUTAKIWA HUGAWANYWA NDOA INAPOVUNJIKA.
Ndoa inapotangazwa kuvunjika mali ambazo hupaswa kugawanywa ni
mali za wanandoa wenyewe. Swali mbele yetu ni kuwa ni zipi mali za
wanandoa. Mali za wanandoa ni zile mali zote zilizochumwa na
wanandoa hao kwa jitihada au juhudi za pamoja wakati wa ndoa
yao. Mali hizo zaweza kuwa zinahamishika au hazihamishiki.
Mali
zisozo hamishika ni kama nyumba, viwanja, mashamba n.k. Mali
zinazohamishika ni kama magari, baiskeli, pikipiki,vifaa vya ndani
kama fenicha, fedha benki, na mali nyingine ambazo hazionekani kwa
macho au hazigusiki kama hisa n.k. Zingatia sana usije kudhulumiwa
kwa kuwa hata hisa pamoja na akiba ya fedha benki nayo ni mali
inayostahili kugawanywa.
2. JE MALI ILIYOPATIKANA KABLA YA NDOA
HUGAWANYWA.
Mali zilizopatikana kabla ya ndoa haziwezi kugawanywa ndoa
inapovunjika isipokuwa tu kama zilibadilishwa kuwa za wanandoa
wakati wa ndoa. Swali ni zinawezaje kubadilishwa kuwa za wanandoa.
Zinabadilshwa kuwa za wanandoa iwapo wanandoa walikubaliana kwa
makubaliano maalum kuwa mali kadha wa kadha zitakuwa zetu wote.
Na hii inaweza kuwa kwa maandishi au kwa kubadili majina ya
nyaraka za umiliki na kuzifanya kuwa na majina yote mawili ya
wanandoa kutoka la mmoja la awali. Lakini pia zaweza kuwa za kwao
wote kimatendo, kwa mfano kabla ya ndoa mmoja wa wanandoa
alikuwa na nyumba lakini haijamaliziwa.
Thubutu!! sio wanaume wa Kitanzania hasa inapotokea mume amefariki. Hao ndugu wanatamwambia mwanamke wewe kwanza ulikuwa hufanyi kazi. Wanachukua mali zote.
ReplyDeleteMfano, familia moja baba ni daktari mama ni mhandisi. Wote wanachangia uchumi wa familia. Wagawane kwa kiwango walichochangia kulingana na mishahara yao.
ReplyDeleteFamilia nyingine, mama ni mhandisi, baba hana ujuzi wa kazi yoyote hivyo hubaki nyumbani. Atagawana vipi wakati hakuwa na uwezo wa kuzalisha mali wala hakuchangia kama mwenzake hapo juu.
Mi nadhani kwa hao wabaki nyumbani kama ni kwa makubaliano lakini uwezo wa kuzalisha mali wanao basi wanaweza kugawana.
Maisha ni kusaidiana kuzalisha mali. Kutegemea mtu mmoja kuzalisha mali na watu wengi kutumia ndo maana hatuendelei. Enyi mlo na uwezo wa kuzalisha mali kwa sababu mlijiandaa kwa kusoma na kupata ujuzi, mnaweza kuepuka shida za talaka kwa kuoana na wenye ujuzi wenzenu. Kwani waso na ujuzi huwapenda "bread winners" na kwa fujo za talaka ndo wao zama wakitaka "economic independence"
sisi kwetu mali ni ya ukoo si ya watu wawili.
ReplyDeleteSheria ya pre-nup inahitajika hapa ili kudhibitisha mapenzi halisi.
ReplyDeleteMaana hakuna sheria inayolinda mali ya mwanandoa.
Ndiyo mama wa nyumbani anastahili nusu ya mgao uliopatikana katika ndoa hii. Mambo ya kusema hakuchangia hayapo alipokuwa anakupikia na kukufulia kwani hakukuneemesha ili ukatafute hiyo mali?
ReplyDeleteKupika. Ntaondoa hoja yako kwa kuajiri hausgeli. Atafua atapika atadeki. huyu mama/baba wa nyumbani utetezi wake ni upi? Mapenzi hayauzwi ni hiari.
ReplyDeleteNapenda hii mada iende ukurasa wa mbele ili nione uchangiaji.
I see this law is driven by emotion (pity and sympathy). It contradicts principles of economics. Eventually, it will destroy families like it did in USA.
ReplyDeleteLazy people will target to marry the rich, no love, after few years they want divorce so they can collect their share and start a business. This law will ruin morality. Marrying the rich will become a legal economic activity.
wengi wa hao wakaa nyumbani huwa hawana ujuzi wa kukusaya mali kabla na wakati wa ndoa. Kwanza ndoa ndo maponeo yao. Nyie mnasema kasakrifice maisha yake. hakuna.
ReplyDeleteHapo wasomi itabidi waendane na wasomi wenzao kuepuka matatizo.
Hii sheria ikifikiriwa vizuri itafanya wenye nacho kuwabagua wasonancho wakati wa kutafuta mchumba.
ReplyDeleteYeeni imewekwa hela kwa ajili ya kusomesha watoto halafu inabadhiriwa ili mradi igawanwe?
ReplyDeleteHiyo maana mnayoona pana ndo finyu hasa maana haiangalii kanuni za uchumi wala hisa za watoto.
kama kulikuwepo na zamu za kufanya kazi za nyumbani basi inabidi wasigawane kwani mama hakuchangia hela na baba aliosha vyombo, kudeki, kufua, kupika, n.k. pia.
ReplyDeleteKwa nje, hii sheria inamtetea mwanamke. Kwa ndani, hii sheria imemwangusha mwanamke katika nchi kubwa. masichana haoni sababu ya kusoma saan ikiwa kuna wasiosoma wamedaka jamaa mwene fucha nzuri, wakatalikiwa na sasa wanazo noti.
ReplyDeleteMnawafundi hilo. hisia si njia nzuri ya kutunga sheria.
Mfanyakazi akipata ajali ya gari, hupata fidia ya lost wages kwa siku ambazo hakwenda kazini kwa sababu ya ugonjwa uloletwa na ajali. uthibitisho wa kiasi cha fidia ni paystub ya kila mwezi kabla ya ajali.
ReplyDeletewa nyumbani akipata ajali hana fidia ya lost wages kwani hana paystub.
Huu ni uthibitisho wa kiuchumi siyo kihisia tuu.