Na Bashir Yakub.
Watu wengi wamenunua viwanja/nyumba lakini mali hizo zimeendelea kubaki katika majina ya waliowauzia. Wapo ambao imepita hata miaka kumi tangu wanunue maeneo lakini bado hawajabadili jina kuingia jina lake. Zipo sababu nyingi zinazosababisha hali hiyo lakini moja ni watu kutokujua umuhimu wa kubadili jina kwa haraka.
Hapa sizungumzii tu kubadili jina isipokuwa nazungumzia kubadili jina kwa haraka. Kupitia makala haya napenda kuwaamsha watu kuhusu umuhimu mkubwa wa kubadili jina kwa haraka iwapo umenunua nyumba/kiwanja kwa mtu. Ni muhimu sana kufanya hivyo na itakuepusha na mambo mengi.
1.KAMA HUJABADILI JINA ALIYEKUUZIA BADO NDIYE MMILIKI.
Ikiwa kutatokea mgogoro wa umiliki wakati ambao umenunua nyumba/kiwanja na hujabadili jina kwenda kwenye jina lako kuna hatari kubwa zaidi ya kupoteza ulichonunua. Hii ni kutokana na ukweli kuwa utapokuwa unatatuliwa mgogoro wa nani mmiliki swali la kwanza huwa ni nani ambaye nyaraka ya umiliki ina jina lake.
Yule ambaye jina lake linaonekana kwenye hati au leseni ya makazi ndiye hupewa kipaumbele na kwa mujibu wa sheria mwenye jina kwenye hati au leseni ya makazi ndiye mmiliki. Wewe uliyenunua utakuwa na mkataba na jina lako litakuwa kwenye mkataba lakini pamoja na kuwa na jina kwenye mkataba bado huwezi kulinganisha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...