LIB4 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji Bi.Fatuma Janga na baadhi ya majeruhi wakati alipowatembelea jana Feb 17, 2014 baada ya kuangukiwa na nyumba zao kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha juzi kijijini  hapo. 
LIB1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (wa pili kulia), Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli na baadhi ya Viongozi, wakati alipowasili Kitongoji cha Mnazi Mmoja, Msoga jana kwa ajili ya kuwafariji wananchi waliokubwa na maafa kwa kuangukiwa na nyumba zao  kutokana na Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha juzi. Katika tukio hilo jumla ya watu 12 walijeruhiwa na jumla ya nyumba 128 kubomoka. Picha na OMR
LIB2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (kulia), wakati alipowasili Kitongoji cha Mnazi Mmoja, Msoga jana kwa ajili ya kuwafariji wananchi waliokubwa na maafa kwa kuangukiwa na nyumba zao kutokana na Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha juzi. Katika tukio hilo jumla ya watu 12 walijeruhiwa na jumla ya nyumba 128 kubomoka. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli (kulia) wakiongozwa na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto),  baadhi ya Viongozi, wakati alipowasili Kitongoji cha Mnazi Mmoja, Msoga jana kwa ajili ya kuwafariji wananchi waliokubwa na maafa kwa kuangukiwa na nyumba zao kutokana na Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha juzi. Katika tukio hilo jumla ya watu 12 walijeruhiwa na jumla ya nyumba 128 kubomoka. Picha na OMR .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ule msemo wa kunusuru kaya maskini una malengo gani? miye huwa siuelewi kabisa. Mbona bado hatuoni maendeleo ya kunusuru kaya maskini na viongozi wanaosimamia hiyo program kuonekana kama wanafanikiwa. Hii ndo inakuwaje sasa, mie siielewi. Maana watu bado wapo kwenye kaya za ajabu sana.

    ReplyDelete
  2. Ningependa kusaidia kujenga nyumba tatu za walioathirika wale tu wasiojiweza kiuchumi wazee na kinamama wajane. Je ni nani mratibu? na anapatikana wapi. Mdau Joshefu Dar. Wadau wengine harambee tuwasaidie wenzetu waliopata majanga.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...